Featured Kitaifa

BAHI YATOA MIKOPO YA SH. MILIONI 104 KWA WAJASIRIAMALI

Written by mzalendoeditor

HALMASHAURI ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani imekabidhi vifaa/ mikopo yenye thamani ya Sh. Zaidi ya Milioni 104 kwa vikundi 18 vya uzalishajimali vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu ili kuviwezesha kujikwamuwa kiuchumi.

Akikabithi mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani humo Mwanahamisi Munkunda amewataka wanawake kutumia Fedha hizo kwa lengo lililokusudiwa Na si vinginevyo .

‘’Wanawake wengi ni waaminifu lakini wanashindwa kurudisha mikopo kutokana akishatoka kuchukua mkopo akifika nyumbani baba anamwambia lete hiyo hela kuna dili Fulani nikalipige nitapata hata milioni nane mwishowe anashindwa kurudisha rejesho na hela anaenda kuolea mke wa pili hiyo ndo changamoto kubwa ,’’ alisema Mkuu huyo.

Pamoja Na hayo Munkunda amewata Wajasiriamali hao kuchamkia Fursa zilizopo katika wilaya hiyo ikiwemo minada za kila Mwezi za wilaya, Kilimo cha mpuga ili kuhakikisha wilaya hiyo iinajitambulisha kwa kuwepo kwa kitu cha tofauti Na cha pekee .

Awali akiwasilisha taarifa ya mikopo hiyo Afisa Maendeleo ya jamii ya wilaya ya Bahi Denis Komba amesema changamoto zilizopo ni pamoja Na madeni Sugu kwa baadhi ya Vikundi kutorejesha mikopo kwa wakati hasa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu Na kudai kuwa jitihada za ufuatiliaji wa mara kwa mara kwa kuvitembelea ilimkuangalia uhai wa miradi yao na mipango yao juu ya ulipaji wa deni.

Naye Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Bahi sterwart Masima amewataka wajasiriamali Hao kubadili Fikira Na kuacha kufanya biashara kwa mazoea na matokeo yake wajipambanue ili kuweza kuibadilisha wilaya hiyo kiuchumi .

Nao Baadhi ya Wajasiriamali waliopokea Mikopo Na vifaa hivyo akiwemo Deogratius John mhasibu kikundi cha TUNAWEZA WALEMAVU Bahi Makulu wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwajali watu wenye uhitaji Na kuwataka wajasiriamali wenzao kufanayakazi kwa bidii na kuiomba tena Serikali kuwatafutia masoko ili Bidhaa wanazozidhalisha ziweze kuuzika kwa lengo la kuzisaidia familia zao ziweze kupata mahitaji ya Msingi ikiwemo kusomesha Watoto.

Kupitia fedha za marejesho Halmashaurikwa kipindi cha mwaka wa utekelezaji imewezesha jumla ya mikopo yenye thamani ya shilingi Zaidi ya milioni 118,kwenye jumla ya vikundi 26 aidha kiasi cha Shilingi Zaidi ya milioni 13 zilikopeshwa robo ya kwanza.

About the author

mzalendoeditor