Featured Kitaifa

WADAU WANAOTEKELEZA PROGRAMU JUMUISHI YA MALEZI,MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA MATOKEO YALIYOKUSUDIWA

Written by mzalendoeditor

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju akijadiliana na timu ya wataalam kutoka Mtandao wa Maendeleo ya Awali ya Mtoto (TECDEN), shirika la Children in Crossfire na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania wakati wa kutambulisha mradi wa MTOTO KWANZA unaolenga kuimarisha huduma kwa watoto wa madarasa ya awali nchini, leo tarehe 03/03/2022 katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma

Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Children in Crossfire CiC-Craig Ferla akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa MTOTO KWANZA utakaosaidia kuimarisha huduma kwa watoto wa madarasa ya awali nchini, leo tarehe 03/03/2022 katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku akielezea utekelezaji wa Program ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto kutambulisha mradi wa MTOTO KWANZA utakaosaidia kuimarisha huduma kwa watoto wa madarasa ya awali nchini, leo tarehe 03/03/2022 katika ofisi za Wizara jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Mtandao wa Maendeleo ya awali ya mtoto Mwajuma Rwebangira akifafanua jambo wakati wa kutambulisha mradi wa MTOTO KWANZA utakaosaidia kuimarisha huduma kwa watoto wa madarasa ya awali nchini, leo tarehe 03/03/2022 katika ofisi za Wizara jijini Dodoma

………………………………………………………..

Na MJJWM, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amewataka wadau wanaotekeleza Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kuhakikisha wanafanya kazi kwa matokeo yaliyokusudiwa.

Mpanju ametoa kauli hiyo jijini Dodoma leo tarehe 03/03/2022, wakato akipokea mradi wa “Mtoto Kwanza” uliotambulishwa na Mtandao wa Malezi ya Awali ya Mtoto (TECDEN) kwa kushirikiana na Shirika la Children in Crossfire na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari UTPC wenye lengo la kuboresha utoaji wa elimu ya awali kuwa na viwango vinavyohitajika kuwakuza watoto.

“Tukiona hakuna watoto waliotelekezwa, watoto wanaoishi mitaani wanakwisha, tutajua kazi imefanyika” amesema Mpanju.

Aidha Mpanju amewapongeza wadau hao kwa kuunga mkono juhudi za Serikali na kuwa sehemu ya kutekeleza malezi na makuzi ya watoto na

Akieleza lengo la mradi huo, utakaotekelezwa kwa miaka mitatu, Mkurugenzi wa Mtandao wa Maendeleo ya Awali ya mtoto (TECDEN) Mwajuma Rwebangira, amesema mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto iliyozinduliwa kwa ushirikiano na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum mwezi Novemba mwaka jana.

Ameongeza Mradi huo utakaogharimu shilingi za Kitanzania Billioni 7 kwa ufadhili wa Conrad Hilton utatekelezwa kwa kushirikiana na Shirika la Children in Crossfire na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na unalenga kuwafikia watoto katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.

About the author

mzalendoeditor