Rais wa Heshima wa klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji’ (Moodewji) ametoa pole kwa Ghalib Said Mohammed (GSM) kufuatia msiba wa Baba yake mzazi, Mzee Said Mohamed.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Mo amendika “Mimi, pamoja na familia ya Simba, tunatoa pole sana kwa Ghalib Said Mohamed, kwa kupata msiba wa baba yake.
“Marehemu Mzee Said alikua ni mfanyabiashara mkubwa mwenye mafanikio. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema. GSM, kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu”
Mzee Said Mohamed alifariki usiku wa kuamkia jana Machi 1, 2022 na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.