Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AELEKEA NCHINI KENYA

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiagana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma katika uwanja wa ndege wa Dodoma wakati akiondoka nchini kuelekea Nairobi nchini Kenya kushiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Kimataifa la Mazingira unaoenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP). Machi 2,2022.

……………………………………………

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 2 Machi 2022, ameondoka nchini kuelekea Nairobi nchini Kenya ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Maalum wa Baraza la Kimataifa la Mazingira unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4, Machi 2022.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo ni maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP),ukilenga kujadili na kupata maamuzi ya pamoja katika hatua za mwanzo za kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki. 

                                    

About the author

mzalendoeditor