Mkufunzi mmoja aliyejulikana kwa jina la Tom Mansfield amefariki dunia baada ya kunywa kafeini ambayo ni sawa na vikombe 200 vya kahawa.
Mkufunzi huyo alitumia kimakosa kiasi cha kafeini alichotakiwa kutumia kwenye mizani ya jikoni.
Uchunguzi umebaini kuwa Bwana Mansfield alikuwa akilalamikia maumivu ya kifua na mapigo ya moyo wake kwenda haraka baada ya kunywa kinywaji hicho.
wataalam wameonya kwamba kuna hatari endapo mtu atakunywa zaidi ya kiasi kilichopendekezwa.