Featured Michezo

SIMBA YASHINDWA KUTAMBA UGENINI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Written by mzalendoeditor

Na Alex Sonna

WAWAKILISHI Pekee wa Afrika Mashariki na Kati Timu ya Simba imeshindwa kutamba ugenini baada ya kuchapwa mabao 2-0 na wenyeji RSB Berkane Mchezo wa Kundi D Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mchezo uliopigwa uwanja wa Stade Municipal de Berkane nchini Morocco.

RSB Berkane walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Adama Ba  akitumia vizuri mpira wa adhabu (Faulo) dakika 32 akipiga na kwenda wavuni moja kwa moja na kumuacha Aishi Manula hana la kufanya.

Mnamo dakika ya 41 Charki El Bahri aliifungia Berkane bao la pili kwa kichwa akitumia vizuri kona iliyopigwa na Badri hadi mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko huku Simba wakianza kwa kasi na ya kutafuta bao.

Kwa ushindi huo RSB Berkane wamefikisha Pointi 6 na kupanda hadi kileleni mwa msimamo wa kundi hilo,Simba wanabaki nafasi ya pili wakiwa na Pointi 4,US Gendarmerie wakishika nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 4 huku ASEC Mimosas wakiburuza Mkia wakiwa na Pointi 3.

Mchezo mwingine wa kundi hilo US Gendarmerie wameutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kuichapa mabao 2-0 ASEC Mimosas kwa mechi hizo timu zote zimemaliza mzunguko wa kwanza na zitaanza kurudiana mwezi wa tatu mwaka huu.

About the author

mzalendoeditor