Featured Kitaifa

WIZARA YA AFYA YAKABIDHI MASHINE ZA KUCHANGANYA CHUMVI NA MADINI JOTO TAMISEMI.

Written by mzalendoeditor

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof.Abel Makubi ,akizungumza wakati kukabidhi mashine tano za kuchanganya madini joto kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe,akiishukuru Wizara ya Afya kwa kuwakabidhi mashine tano za kuchanganya madini joto kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Caroline Nombo,akizungumza wakati kukabidhi mashine tano za kuchanganya madini joto kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe nchini(TFNC), Dk.Germana Leyna,akielezea lengo la kukabidhi mashine tano za kuchanganya madini joto kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Nutrition International Dkt. Daniel Nyagawa ,akizungumza wakati kukabidhi mashine tano za kuchanganya madini joto kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali  wakati wa makabidhiano ya mashine tano za kuchanganya madini joto kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof.Abel Makubi ,akikata utepe kwa ajili ya kukabidhi mashine tano za kuchanganya madini joto kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof.Abel Makubi akikabidhi nyaraka za mashine za kuchanganyia chumvi na madini joto kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe kwa ajili ya kuwakabidhi Makatibu Tawala wa mikoa ya Pwani, Mtwara na Tanga ili kusaidia kuongeza uzalishaji wa chumvi yenye kiwango cha kutosha cha madini joto hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe, akimkabidhi nyaraka za mashine Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Abdallah mara baada ya kukabidhiwa mashine tano za kuchanganya madini joto zilizotolewa na Wizara ya Afya kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe, akimkabidhi nyaraka za mashine Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya kukabidhiwa mashine tano za kuchanganya madini joto zilizotolewa na Wizara ya Afya kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

MUONEKANO wa  mashine tano za kuchanganya madini joto zilizotolewa na Wizara ya Afya kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.


Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Tumbo,akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhiwa mashine tano za kuchanganya madini joto zilizotolewa na Wizara ya Afya kwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya Halmashauri zinazozalisha chumvi hafla iliyofanyika leo Februari 24,2022 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imekabidhi mashine tano za kisasa za kuchanganya chumvi na madini joto kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI zilizotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kupitia shirika la Kimataifa la Nutrition Intenational kwa ajili ya kusimikwa katika Mikoa ya Tanga, Pwani na Mtwara ili kusaidia kuongeza uzalishaji wa chumvi yenye kiwango cha  kutosha cha madini joto nchini.

Akikabidhi mashine hizo leo Februari 24,2022 jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi  amesema Utafiti uliofanyika nchini mwaka 2019 ulibaini Tanzania inazalisha chumvi Tani 330,712 kwa mwaka na kati ya Chumvi hiyo Tani 141, 22 ambapo ni sawa na asilimia 43 haiwekwi madini joto hivyo ujio wa mashine hizo utasaidia kuongeza uzalishaji wa chumvi yenye madini hayo.

Prof Makubi amesema mashine hizo ambazo zimetengenezwa nchini na wataalamu kutoka VETA zimeweza kugharimu kiasi cha shilingi milioni 55 huku gharama ya mashine moja ikigharamu kiasi cha shilingi milioni 11 na kusaidia kuokoa milioni 14 kwa kila mashine endapo zingeagizwa kutoka nje ya nchi.

“Mwaka 2018 shirika la Nutrition International ilifadhili ununuzi wa mashine tatu zilizoagizwa kutoka Afrika Kusini kwa jumla ya Shilingi milioni 75 ambapo mashine moja iligharimu shilingi Milioni 25 na kusimikwa Halmashauri za Kilwa, Hanang na Meatu na zinaendelea kufanya kazi na safari hii mashine hizo zimeweza kutengenezwa na Watalaam wetu kutoka VETA kusaidia kuokoa shilingi milioni 14 kwa kila mashine” amesema  Prof Makubi.

Hata hivyo Prof.Makubi amezitaka Halmashauri zinazozalisha chumvi kusimamia kikamilifu wazalishaji kuchanganya chumvi na madini joto ili kuondokana na madhara hayo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe, amewataka  Makatibu Tawala wa Mikoa iliyopatiwa mashine hizo kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na sio kuzifungia.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Caroline Nombo, amesema kuwa  kutokana na maboresho ya mafunzo na ufundi stadi nchini, VETA imetengeneza mashine hizo na kuokoa fedha za serikali ambazo zingetumika kununua nje ya nchi.

Amesema kuwa uwepo  wa mashine hizo utasaidia utekelezaji wa mwongozo wa lishe shuleni uliozinduliwa mwishoni mwa mwaka jana.

‘Kutengenezwa kwa mashine hizo na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) imejidhihisha kuwa sasa wahitimu na wanafunzi wa vyuo hivyo vilivyopo nchi nzima sasa wameanza  kutatua changamoto zinazoikabili jamii na wanaweza kutengeneza vitu amavyo vitapatikana kwa gharama nafuu na kuokoa gharama za fedha za serikali endapo bidhaa hizo zitaagizwa nje ya nchi.’amesema Prof.Nombo

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe nchini(TFNC), Dk.Germana Leyna,amesema kuwa lengo la kutoa mashine hizo ni kuhakikisha asilimia 90 ya kaya zitumie chumvi yenye madini hayo.

“Taasisi yetu inatoa elimu na namna ya kuchanganya madini hayo na kupima,  kwa mwaka 2016/17 utafiti wa hali ya lishe unaonesha asilimia 60 ya kaya zinatumia chumvi yenye madini joto na utafiti wa mwaka 2018 ulionesha bado hatujapiga hatua,”amesema Dk.Leyna

Dk.Leyna amesema kuwa Taasisi yao kwa kushirikiana na wadau ilianzisha mchakato wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo ambao utafiti unaonesha ndio wanaochangia kwa kiwango kikubwa kuzalisha chumvi ambayo haina madini joto.

Aidha amesema kuwa  mwaka 2019, zilinunuliwa mashine tatu kutoka Afrika kusini kwa gharama ya Sh.Milioni 25 kila mmoja na kuzisambaza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Nutrition International Dkt. Daniel Nyagawa amesema katika Mpango mkakati wake wa miaka 6 ulioanza mwaka 2018 hadi 2024 shirika hilo limejielekeza kufanya kazi zake kwa karibu na Serikali na Taasisi zake ili kwa pamoja  kuweza kupambana na utapiamlo na madhara yatokanayo na utapiamlo.

Dkt. Nyagawa amesema kwa sasa wanafarijika kuona sasa Mashine hizi zitaweza kupatikana nchini tena chini ya Taasisi ya Serikali hivyo zoezi la ugawaji wa mashine hizi utakuwa endelevu wakati wowote zikihitajika  na kuna uwezekano Tanzania ikavuka asilimia 61 ya kaya zinazotumia chumvi yenye madini joto toshelevu endapo zitatumika kikamilifu.

About the author

mzalendoeditor