Featured Kitaifa

‘ITAFANA SANA USHIRIKI WA TANZANIA MAONESHO YA DUBAI 2020 EXPO’-DK.KIJAJI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Kushoto) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Uwekezaji, Mhe. Mudrick Ramdahan Solaga (Kulia) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara (Katikati) Februari 23, 2022 wakati wa kikao cha maandalizi ya Siku ya Kitaifa Tanzania itakayofanyika 26/02/2022 ikifuatiwa na Kongamano la Biashara na Uwekezaji ambalo litafanyika tarehe 27 Februari, 2022.

Kamishina Generali wa Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Expo2020 Dubai Mhe. Balozi Mohamed Mtonga akielezea hatua za maandalizi Februari 23, 2022 wakati wa kikao cha maandalizi ya Siku ya Kitaifa Tanzania itakayofanyika 26/02/2022 ikifuatiwa na Kongamano la Biashara na Uwekezaji ambalo litafanyika tarehe 27 Februari, 2022.

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu akielezea hatua za maandalizi Februari 23, 2022 wakati wa kikao cha maandalizi ya Siku ya Kitaifa Tanzania itakayofanyika 26/02/2022 ikifuatiwa na Kongamano la Biashara na Uwekezaji ambalo litafanyika tarehe 27 Februari, 2022.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu

……………………………………………….

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akiwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Bw. Omar Shaaban wakiwa ,Dubai wameongoza kikao cha maandalizi ya Siku ya Kitaifa ya Tanzania itakayofanyika 26/02/2022 wakati wa Maenesho ya EXPO2020 Dubai.

Pia kutakuwa na  Kongamano la Biashara na Uwekezaji ambalo litafanyika tarehe 27 Februari, 2022 ambapo Mgeni Rasmi wa Siku hiyo  ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa siku hiyo, iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) itafanyika wakati wa Maenesho ya EXPO2020 yaliyoanza 1 Oktoba, 2021 hadi 31 Machi, 2022 ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi 192 zinazoshiriki Maonesho hayo.

”Katika siku hiyo, Rais Samia anatarajia kufanya mazungumzo na Uongozi wa Serikali ya UAE kwa lengo la kukuza mahusiano ya kiuchumi na kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili na kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii.”amesema 

Aidha, Kongamano litakalofanyika litahudhuriwa na Wafanyabiashara kutoka Tanzania, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na nchi Washiriki wa EXPO2020 Dubai. Kongamano hilo litakutanisha Wawekezaji, Wauzaji na Wanunuzi wa bidhaa mbalimbali, na Taasisi za Kimataifa za Fedha katika jukwaa moja. Serikali ya Tanzania inatarajia kunadi Miradi ya Kimkakati kutoka Sekta za Viwanda, Kilimo, Madini, Utalii, Nishati, Miundombinu, Uchumi wa Buluu, Mawasiliano, Ujenzi, Afya, Uchukuzi na Elimu.
Tanzania inatumia fursa ya Maonesho hayo kutafuta masoko ya uhakika na endelevu ya bidhaa zitokanazo na mazao ya kimkakati kama vile kahawa, korosho, chai, mkonge, karafuu, pareto, viungo, mwani, nyama, Samaki na bidhaa nyingine zinazohitajika kwenye soko la kimataifa.

About the author

mzalendoeditor