Featured Michezo

FOUNTAIN GATE PRINCESS YATAMBA KUIPOKONYA SIMBA QUEENS UBINGWA WA LIGI YA WANAWAKE

Written by mzalendoeditor
Na.Alex Sonna,DODOMA
TIMU ya Fountain Gate Princess imetamba kuipokonya Simba Queens Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) Msimu wa 2021/2022 kutoka na ubora wa kikosi hicho.
Akizungumza na Mzalendo.co.tz Afisa habari wa timu hiyo Timotheo Francis amejinasibu kuwa msimu huu lazima wachukue ubingwa kutokana na ubora wa wachezaji waliosajiliwa katika kikosi hicho.
‘Tumesajili vizuri kikosi chetu kinajumuisha wachezaji kutoka mataifa manne Tanzania,Kenya,Congo na Burundi na wachezaji wetu wamekuwa msaada katika mataifa hayo katika timu zao za Taifa huku ligi ikiwa imesimama wachezaji 7 wameitwa katika kikosi cha Tanzania U17’amesema Bw.Timotheo Francis 
 
Fountain Gate Princess katika msimamo wa Ligi hiyo wanashika nafasi ya tano wakiwa na pointi 16 kwa michezo saba huku wakiwa wameshinda mechi 5,sare moja huku wakiwa wamepoteza mechi moja.
Hata hivyo Bw.Timotheo Francis  amesema kuwa Fountain Gate Princess ni timu iliyowekeza zaidi kuliko timu yoyote inayoshiriki Ligi hiyo wakiwa na wadhamini watatu ambao ni Fountain Gate School,Uba Bank pamoja Gedli Security hivyo wanastahili kuwa mabingwa msimu huu.

About the author

mzalendoeditor