Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya wameendelea kuwasha moto katika Michuano hiyo baada ya kuibuka na shindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lille ya Ufaransa katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Stamford Bridge Jijiji London.

Mabao ya Chelsea yamefungwa na Kai Havertz dakika ya nane na Christian Pulisic dakika ya 63 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya Robo Fainali.

Chelsea kama itaweza kutoka sare au kushinda mechi ya marudiano moja kwa moja itatinga Robo Fainali ya Michuano hiyo.

Mechi nyingine Villarreal imeshindwa kutamba katika uwanja wake baada ya kulazimishwa sare ya kufunga bao 1-1 na Juventus ya Italia.

Previous articleLIVE:RAIS SAMIA AKIFUNGUA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE KIBAHA – PWANI
Next articleRAIS SAMIA AZINDUA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE KIBAHA – PWANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here