WANAWAKE katika vijiji vya Lyamidati na Lyabukande wilayani Shinyanga , wamelalamikia kitendo cha madadapoa maarufu ‘machangudoa’ kutoka mjini kwenda huko kipindi cha mavuno, kufanyabiashara ya kujiuza kwa kubadilishana na zao la mpunga.
Walisema hali hiyo inasababisha familia zao kukosa chakula kwa kuwa wanaume wananunua madadapoa hao kwa kuwapa mpunga.
Wanawake hao kutoka vijiji vya Lyamidati na Lyabukande wilayani Shinyanga, walipaza sauti hizo juzi kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa namna ya kupambana na matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, yaliyotolewa na Shirika la Agape.
Mmoja wa wanawake hao kutoka kijiji cha Lyamidati, Matha Malale, alisema kipindi cha masika familia zao zinakuwa na upendo, lakini msimu wa mavuno ukifika migogoro inaanza kuibuka.