KOCHA Mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp JURGEN Klopp amempongeza mshambuliaji wake hatari kutoka Misri Mo Salah kwa kufikisha mabao 150.

Mchezaji huyo amekuwa kwenye kiwango bora zaidi tangu atue katika klabu hiyo na  alifunga katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Watford na tangu hapo hajaacha kufunga.

Kwa Sasa Salah amefikisha mabao 150 katika mechi 233, na ameweka rekodi ya kuwa na uwiano bora zaidi wa mabao ukilinganisha na mechi alizocheza, kuliko mchezaji yeyote wa Liverpool kihistoria ambaye ameifungia klabu hiyo mabao zaidi ya 30.

Hii maana yake ni kwamba amefikisha idadi ya mabao 150 kwa haraka zaidi, yaani katika mechi chache zaidi.

“Bao lake la kwanza pale Watford pengine ndilo lilikuwa rahisi zaidi. Alifunga mabao mengine 149 ndani ya kipindi kifupi sana,” alisema Klopp.

“Siwezi kukumbuka mabao yake yote lakini nayakumbuka mengi na kulikuwa na mabao mengine mazuri zaidi. Dhidi ya Chelsea, akifunga kutoka kwenye kona, alipofunga baada ya kukokota mpira dhidi ya Manchester City, dhidi ya United kwa pasi ya Alisson. Na  (juzi) dhidi ya Norwich lilikuwa bao zuri kusema ukweli.”

Salah sasa amekuwa mmoja wa wachezaji 10 tu katika histori

Previous articleWALALAMIKIA ‘MACHANGUDOA’ KUFURIKA MSIMU WA MAVUNO
Next articleKICHWA CHA KWANZA CHA UMEME KWA MAJARIBIO YA RELI YA SGR CHAWASILI NCHINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here