Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki nchini halfa iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Balozi wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya Manfredo Fanti,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki nchini halfa iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Waziri wa Kilimo,Umwangiliaji,Maliasili na Mifugo Zanzibar Bi.Lela Mohamed Mussa,akielezea walivyojipanga kutekeleza mradi huo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki nchini halfa iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Balozi wa Ubelgiji nchini Bw.Peter Van Acker,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki nchini halfa iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi,akitoa taarifa kuhusu programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji Nyuki wakati wa uzinduzi wa Programu hiyo halfa iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali pamoja na washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki nchini halfa iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki nchini halfa iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki nchini halfa iliyofanyika leo Februari 21,2022 jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,DODOMA
WIZARA ya Maliasili na Utalii imezindua Programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki ambao unatakelezwa kwa Euro milioni 10 sawa na Sh bilioni 27.
Akizungumza leo Februari 21,2022,Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Programu hiyo,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja amesema takwimu zinaonyesha kuwa uzalishaji wa asali nchini uliongezeka kutoka tani 4,860 mwaka 1998 za asali hadi kufikia tani 31,179 mwaka 2021 na nta kutoka 1834 mwaka 1998 hadi tani 1894 mwaka 2021.
Amesema kiwango hicho bado ni kidogo na ukilinganisha na fursa ya uzalishaji wa asali nchini ambapo amedai kama nchi kuna fursa ya kuzalisha asali takribani tani 138,000 na tani 9200 za nta kwa mwaka.
Akizungumzia Programu hiyo ya miaka mitano, Mhe.Masanja ameeleza kuwa inafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na itatekelezwa katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Singida, Shinyanga,Tabora kwa upande wa Tanzania bara na kisiwa cha Pemba Zanzibar.
”Bado uchambuzi wa kitaalamu unaendelea wa kubaini wilaya na vijiji vilivyomo ndani ya mikoa hiyo ambapo mradi huu utatekelezwa’amesema Masanja
Amesema programu hiyo itajenga uwezo wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufugaji nyuki pamoja na taasisi zinazosimamia sekta hiyo ya ufugaji wa nyuki.
Mhe.Masanja amesema kuwa program hiyo itakwenda kuimarisha mifumo ya uzalishaji wa mazao ya nyuki, kuwezesha maeneo ya uchakataji na uongezaji wa thamani wa mazao ya nyuki.
Amesema programu hiyo itawezesha taasisi ya utafiti wa nyuki kuweka vitendea kazi katika maabara ya utafiti wa nyuki iliyopo Njiro mkoani Arusha.
Kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi amesema program hiyo itawezesha kuboresha mifumo mbalimbali ya kibiashara ili kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wa mazao ya nyuki.
“Itaimarisha na kukuza ujuzi kwa watoa huduma za kibiashara na kuboresha uwezo wa wachakataji, wasindikaji na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki ili waweze kusimamia, kukuza na kusafirisha mazao yao hayo,”amesema
Naye, Balozi wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya Manfredo Fanti amesema soko la asali kwa nchi za Ulaya ni kubwa na bado wanahitaji kiasi kikubwa kutoka Tanzania.
Amesema hiyo ndiyo sababu ya kuwekeza fedha nyingi katika sekta hiyo ambazo ni msaada na siyo mkopo.
Amesema kuwa hakuna kiwango kamili kinachotakiwa kupelekwa huko isipokuwa ubora wa asali ndiyo utakuwa kigezo cha kutazamwa na watu wa Ulaya.