Featured Kimataifa

MDUDU MWENYE JINSIA MBILI HUYU HAPA

Written by mzalendoeditor

Mdudu jamii ya panzi maarufu kama mdudu kijiti aliyekuwa akitunzwa amemshangaza mmiliki wake baada ya kugundua kuwa ni nusu mwanaume, nusu mwanamke kitaalamu hujulikana kama gynandromorph.

Wataalamu katika Makumbusho ya historia ya asili walithibitisha kuwa ilikuwa mdudu wa kwanza wa aina hiyo kuripotiwa kuwa na sifa za kike na kiume ‘gynandromorph’ kwa pamoja.

Mmiliki wake Lauren Garfield amewapa jumba la makumbusho la London mdudu huyo kwa ajili ya utafiti wa kisayansi.

About the author

mzalendoeditor