Featured Michezo

VIGOGO SIMBA WAPANDIA DAU POINTI SITA CAF,WAPANGUA FITINA ZA US GENDARMERIE

Written by mzalendoeditor

Tumejipanga tumejipanga hii ni kauli ya Viongozi wa Simba SC ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mabosi wa Simba wakiongozwa na Rais wa Heshima, Mohammed Dewji ‘MO’ wameweka mezani dau la kutosha kuhakikisha mastaa wao wanavuna pointi sita ugenini.

Simba watatupa karata yao ya pili majira ya saa moja usiku  kucheza na wenyeji wao US Gendarmerie ya Niger kwenye Uwanja wa Général Seyni Kountché, Niamey nchini Niger.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema kuwa wamejipanga kuondoka na pointi tatu dhidi ya wenyeji kutokana na benchi la ufundi kuwasoma wapinzani wao walipocheza na RS Berkane na kufungwa mabao 5-3.

Huku viongozi hao wakidai kuwa tayari wamepangua fitina za wenyeji kueleka katika mchezo huo.


“Lakini pia sisi kama uongozi 
tumeifanya kazi yetu ipasavyo, kama mnavyojua tayari tulitanguliza mashushushu wetu kwa ajili ya kukamilisha maandalizi yote na hilo limekamilika.

“Bodi ya Wakurugenzi kwa kushirikiana na Rais wetu wa heshima, MO Dewji kama ilivyo kawaida, imetenga fungu la motisha kwa wachezaji, tunaamini kwa maandalizi tuliyoyafanya tutarudi na ushindi wa kishindo.” 

Taarifa zinasema kwamba, vigogo hao wa Simba, wametenga dola 100,000 (sawa na Sh 230,677,000) kila Simba ikipata ushindi katika michuano hiyo ya kimataifa msimu huu.

Mara baada ya kumaliza mchezo huo Simba wataelekea nchini Morocco kucheza mchezo wao wa tatu dhidi ya RS Berkane, mechi  itakayochezwa Februari 27, mwaka huu.

About the author

mzalendoeditor