Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Benjamin Kuzaga akiwaonyesha waandishi wa habari, silaha aina ya gobore iliyotengemezwa kienyeji na kukamatwa Wilayani Kiteto.

…………………………………………………….

Na Mwandishi wetu, Kiteto

JESHI la polisi Mkoani Manyara linamshikilia mkazi wa kata ya Hale Wilayani Korogwe Mkoani Tanga Omary Mohamed Chuma (52) kwa tuhuma za kufanya uhalifu akitumia silaha haramu.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP) Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea Februari 15 saa 6 mchana katika kitongoji cha Losoiti kijiji cha Asamacha Kata ya Sunya Wilayani Kiteto.

Kamanda Kuzaga amesema Chuma ambaye ni mkulima na mkazi wa Hale alikamatwa na polisi wa doria akiwa na silaha hiyo haramu aina ya gorobe bila ya kibali kwenye kata ya Sunya.

Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa anatumia silaha hiyo aina ya gorore hiyo yenye namba batili HD788-06 bila kibali kwa lengo la kufanyia uhalifu wilayani Kiteto.

“Silaha hiyo haramu iliyotengenezwa kienyeji ikiwa na stakabadhi ya bandia 241519 iliyotolewa June 27 mwaka 2016 wilayani Handeni mkoani Tanga,” amesema kamanda Kuzaga.

Amesema mtuhumiwa huyo anayeshikiliwa kwenye kituo cha polisi wilayani Kiteto, anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika.

“Natoa wito kwa wananchi wote wanaotumia silaha zisizo na vibali wasalimishe kwenye vituo vya polisi popote walipo kwani bila hivyo polisi watawachukulia hatua,” amesema kamanda Kuzaga.

Previous articleMTAKA AZINDUA ZOEZI LA UPANDAJI MITI WILAYANI MPWAPWA,ATOA MAAGIZO MAZITO
Next articleVIGOGO SIMBA WAPANDIA DAU POINTI SITA CAF,WAPANGUA FITINA ZA US GENDARMERIE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here