Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwaongoza wananchi kupanda miti katika eneo la shule ya Msingi Kingiti wilayani Mpwapwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akikitunza kikundi cha ngoma cha Kata ya Kingiti wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza na wananchi wa kata ya Kingiti wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akisisitiza jambo zaidi kwa wananchi wa kata ya Kingiti wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Mpwapwa Mwanahamisi Ally,akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Mwenyekiti wa CCM halmashauri Mpwapwa George Fulme,,akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Muwezeshaji wa Vikundi vya SAT Bi.Flora Romani akisoma risala wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Mkuu wa Ofisi Ndogo ya Shirika la Mpango Chakula Duniani (WFP),Nima Sitta,akielezea mradi wa kilimo himilivu cha zao la Mtamawakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Meneja Mradi wa Kilimo himilivu cha zao la Mtama Bw.William Mwakyami,akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Wananchi pamoja na wanafunzi wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akipanda miti katika eneo la shule ya Sekondari ya Kingiti wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wakiendelea kupanda miti katika eneo la Shule ya Sekonadri ya Kingiti wakati wa uzinduzi wa zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akikabidhiwa zawadi ya Mbuzi na wananchi wa Kata ya Kingiti mara baada ya kuzindua zoezi la kupanda miti katika wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,uliofanyika jana Februari 19,2022.
………………………………………
Na.Alex Sonna,MPWAPWA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amezindua upandaji miti mkoani humo huku akiagiza kila Mwanafunzi kuhakikisha anakuwa na mti wake shuleni ili kuijanisha Dodoma.
Mtaka aliyasema hayo jana Februari 19,2022 wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti na kuhamasisha kilimo cha mtama katika kijiji cha Kingiti wilayani Mpwapwa.
Alisema Maofisa Elimu wahakikishe miti inafika kila shule na kwamba kampeni inalenga kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa na mti.
“Hakikisheni mwanafunzi shuleni anasoma, ana eneo la kufanya usafi, mti anaoutunza, kuwa na bustani ya shule ili kupata elimu ya kupanda miti na utunzaji mazingira, nataka kuona vijiji Dodoma vyenye miti ya kivuli, miti chakula tupande miti yenye faida,”alisema.
“Nataka tutengeneze kijiji tajiri cha mfano, shule tajiri kijiji tajiri, watu tajiri kwa kupanda miti ya matunda na kivuli, pia WFP inahamasisha mlime mtama limeni kwa wingi,”alisema.
Aliwataka Mameneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha miti inapandwa kwenye barabara zinazojengwa na kuwataka wananchi kuondokana na tabia ya kupanda miti kiholela.
“Suala la kupanda miti kiholela tuachane nalo TARURA lazima muoneshe maeneo ya kupanda miti kila Barabara ya TARURA lazima kuonesha eneo la kupanda miti,”alisema.
Hata hivyo, alisema hayupo tayari kuona Halmashauri inakimbizana kutoza wananchi ushuru wa mazao bila kuwekeza kwa kuwapa elimu na kuhamasisha kulima.
“Lazima kutoza kwa unachowekeza huyu anayetoza ushuru anajua maana ya kilimo na kuwa na mashamba, mtu anatoza Sh.1,000 hajui hata mkulima amehangaikaje, kuna siku nitawaambia msitoze, kama hamjawekeza kwenye kufanikisha kukusanya, ni lazima Mkurugenzi kama una vijiji 10 vinakuletea Sh.Bilioni tatu lazima uwekeze.”
“WFP imetoa mafunzo kwa wakulima kulima mtama, sasa idara yako ya kilimo Mkurugenzi imemfundisha nani, Idara yako ya fedha imejiandaaje pale wananchi watakapozalisha mara 10 ya wanavyozalisha sasa au wakizalisha ndo mnaanza kusema hakuna pakuweka tukodi nyumba ya mtu,”alisema.
Alitaka kuhakikisha suala la kuwekeza kwenye kilimo ili wanapokusanya ushuru uwe wenye tija kwao.
Kwa upande wa Mkuu wa Ofisi ndogo ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Nima Sitta, alisema pamoja na kuhamasisha upandani miti pia kuna vijiji 51 vinavyosaidiwa na WFP kupitia mradi wa mtama ambapo mwaka jana ziliuzwa tani 20,000 ambapo kati ya hizo tani 11,000 zilitoka Mpwapwa.
“Kwa Mkoa wa Dodoma kwenye mradi wa mtama tuna vijiji 222 kwenye Wilaya zote na tunategemea mwaka huu tutafikia tani 50,000, kwenye miti tunajitahidi kurudisha ardhi tunayoitumia ambapo tumezalisha miti 62,000 ya asili, 6,000 ya matunda na Mpwapwa hapa wameshapanda miti 17,000,”alisema.