KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Maria Mwakila (26), mkazi wa Kitongoji cha Mbyaso, Kijiji cha Mpunguti, Kata ya Ikama wilayani Kyela mkoani Mbeya, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutokwa na mjusi sehemu za siri alipokwenda kujisadia haja ndogo.
Wiki tatu zilizopita, binti huyo aliripotiwa kujifungua mkono wa mamba na kuzua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.
Ilidaiwa kuwa alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu na alitibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela baada ya kukumbana na mkasa huo.
Siku 18 baada ya kupata matibabu hayo, jana majira ya saa mbili asubuhi, alipokwenda kujisaidia haja ndogo, alidai ulitoka mjusi ukiwa na kucha mkiani.
Akizungumza jana baada ya kumaliza kikao cha machifu, mume wake, Lugano Sindalama, alisema walioana Oktoba mwaka jana baada ya kuwa ameachana na mwanamume aliyekuwa naye wilayani Sumbawanga.