Featured Michezo

GEITA GOLD YAZIDI KUWASHA MOTO LIGI YA NBC ,YAIZAMISHA COASTAL UNION

Written by mzalendoeditor

Timu ya  Geita Gold imeendelea kuutumia vyema uwanja wao wa Nyankumbu baada ya kuwazimisha wagosi wa Kaya Coastal Union kwa kuwachapa mabao 2-0 mchezo uliochezwa  Mjini Geita.

Mabao ya Geita Gold yamefungwa na George Mpole kwa penalti dakika ya 38 na Danny Lyanga dakika ya 41 na kwa ushindi huo, na kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi wa NBC wakiwa na Pointi 20 katika nafasi ya nne.

Coastal Union, wanakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi wakiwa na pointi 17 katika nafasi ya tisa.
Mechi nyingine wa Ligi Kuu leo, wenyeji, Polisi Tanzania wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kagera Sugar inafikisha pointi 20 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya saba, wakati Polisi inafikisha pointi 19 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kukamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi.

About the author

mzalendoeditor