Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwanasiasa ambaye pia ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Antiphas Lissu leo tarehe 16 Februari, 2022 katika Jiji la Brussels nchini Ubelgiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwanasiasa ambaye pia ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Antiphas Lissu leo tarehe 16 Februari, 2022 katika Jiji la Brussels nchini Ubelgiji.

…………………………………………….

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana leo na kufanya mazungumzo mafupi na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Tundu Lissu. 

Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya Rais Samia kukubali maombi ya kiongozi huyo wa Chadema kukutana naye na kuzungumza jijini Brussels.

Aidha katika mazungumzo hayo Mhe. Rais na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, walizungumza masuala mbalimbali yenye maslahi na ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Previous articleWAZIRI NDUMBARO ATOA MAAGIZO MAZITO UGAWAJI WA  VITALU VYA  UWINDAJI 
Next article”TTA SHIRIKIANENI NA SERIKALI KUKUZA MCHEZO WA TENIS’-YAKUBU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here