Featured Michezo Uncategorized

PAMBA FC YATINGA ROBO FAINALI ASFC,YAIZAMISHA DODOMA JIJI

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Pamba FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza (Championship) imetinga hatua ya robo fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuichapa mabao 2-1 Dodoma jiji mchezo uliopigwa uwanja wa  Nyamagana jijini Mwanza.

Mabao ya Pamba FC yamefungwa dakika ya 15 na Mackyada Makolo na bao la pili limefungwa na Malulu Masunga dakika ya 77 huku bao la kufutia machozi la Dodoma jiji likifungwa na Cleophance Mkandala dakika ya 47.

Kwa Matokeo hayo Pamba inaungana na timu za  Yanga,Kagera Sugar,Coastal Union,Geita Gold,Azam FC pamoja na Tanzania Polisi huku timu moja ikisubiriwa kukamilisha idadi ya timu nane.

Mchezo mwingine utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam  Simba watacheza na Ruvu Shooting majira ya saa moja usiku.

About the author

mzalendoeditor