Featured Magazeti

Rais Samia Amteua Kamishna Wa Kazi

Written by mzalendo
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bi. Suzan William Mkangwa kuwa Kamishna wa Kazi.
Kabla ya uteuzi huo, Bi. Suzan alikuwa Mtumishi katika Ofisi ya Rais Ikulu na anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali Francis Ronald Mbindi aliyepangiwa majukumu mengine.
Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Januari, 2022.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

About the author

mzalendo