Featured Kitaifa

BUNGE LA 13 KUANZA RASMI KESHO JIJINI DODOMA

Written by Alex Sonna

MKUTANO wa kwanza wa Bunge la 13 unatarajiwa kuanza rasmi kesho, Novemba 11, 2025, jijini Dodoma.

Mkutano huo unafanyika kufuatia kukamilika kwa shughuli za Uchaguzi Mkuu na tangazo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuitisha Bunge hilo, lililotolewa kupitia Gazeti la Serikali.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, wabunge wateule walipatiwa nafasi ya kujisajili kuanzia Novemba 8 hadi 10, 2025, ambapo zoezi hilo linakamilika leo, Novemba 11, 2025.

Kuanza kwa mkutano huo kutahusisha shughuli mbalimbali muhimu, ikiwemo kuapishwa kwa wabunge wateule, uchaguzi wa Spika na Naibu Spika wa Bunge, kuthibitishwa kwa jina la Waziri Mkuu, pamoja na uzinduzi rasmi wa Bunge jipya.

About the author

Alex Sonna