Featured Kitaifa

NM-AIST NA  ESCSA ZASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA TAFITI ZA AFYA NA TEKNOLOJIA 

Written by Alex Sonna

 

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto) na Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini( ECSA) Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia,) wakisaini hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika Afya leo Oktoba 28,2025.

…..

TAASISI  ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) imesaini hati ya makubaliano na Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA) yenye lengo la kushirikiana katika tafiti, ubunifu na uenezaji wa teknolojia bunifu katika sekta ya afya.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo Oktoba 28,2025, Makamu Mkuu wa Taasisi, Prof. Maulilio Kipanyula, alisema NM-AIST imejikita katika kuzalisha teknolojia bunifu na kufanya tafiti zenye matokeo chanya katika jamii.

Makubaliano hayo yameainisha maeneo kumi ya ushirikiano, yakiwemo tafiti za pamoja, matumizi ya teknolojia za kidijitali katika mifumo ya afya, na kuimarisha ubunifu unaolenga kuzalisha majawabu ya changamoto za kiafya barani Afrika.

“Sisi kama taasisi ya sayansi, teknolojia na ubunifu, tumejidhatiti kuzalisha teknolojia na majawabu yatakayosaidia kuimarisha mifumo ya afya nchini na barani Afrika. ESCAC ipo katika nchi nyingi, hivyo kwa NM-AIST hii ni fursa ya kushirikiana, kujenga mifumo ya afya, na kupeleka majawabu ya kidijitali katika sekta ya afya,” alisema Prof. Kipanyula.

Kwa mujibu wa Prof. Kipanyula, NM-AIST ni taasisi yenye idadi kubwa ya hati miliki (patents) nchini zipatazo 33 ambapo baadhi zinahusiana moja kwa moja na masuala ya afya, ikiwemo teknolojia ya lishe kupitia uji chapchap, mfumo wa kutambua picha za X-ray kwa kutumia akili unde, gauni maalum la theatre, na dripu bunifu inayochanganya mchanganyiko wa dawa kwa wakati mmoja.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa ESCAC, Dkt. Ntuli Kapologwe, alisema makubaliano hayo ni ya kimkakati na yanatarajiwa kuleta matokeo chanya katika muda mfupi, ikiwemo kuanzishwa kwa kituo cha umahiri wa sayansi, teknolojia, ubunifu na utafiti.

“Tumeweka mkazo katika diplomasia ya sayansi na afya, ili nchi wanachama tisa zinufaike na ubunifu wa NM-AIST. Hali ya udumavu katika ukanda wetu ni asilimia 30 hadi 35, hivyo tunahitaji teknolojia za lishe kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema Dkt. Ntuli.

Aliongeza kuwa ushirikiano huo utahusisha pia matumizi ya teknolojia za kidijitali na akili uunde katika utoaji wa huduma za afya, ustawi wa jamii na lishe, sambamba na kuimarisha dhana ya Afya Moja (One Health) kwa nchi zaidi ya 55 barani Afrika.

Kwa sasa, NM-AIST inahudumia wanafunzi kutoka nchi 17 za Afrika, huku ECSA ikijumuisha wanachama kutoka nchi 12, jambo linalotarajiwa kuongeza wigo wa ushirikiano na athari chanya kwa afya ya jamii katika bara zima.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto) na Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini( ECSA) Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia,) wakisaini hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika Afya leo Oktoba 28,2025.

Makamu Mkuu wa NM-AIST, Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto), akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia), ikiwa ishara ya kumbukumbu mara baada ya hafla ya kusaini hati ya makubaliano, Oktoba 28, 2025, Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto), na Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia), wakionyesha hati ya makubaliano baada ya kuiweka saini, Oktoba 28, 2025, Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi naTeknolojia ya Nelson Mandela, Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto) akiongea wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano, Oktoba 28, 2025, Arusha.

Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia), akiongea wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano, Oktoba 28, 2025, Arusha, kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula.

Makamu Mkuu wa NM-AIST, Prof. Maulilio Kipanyula (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia),pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya NM-AIST na ECSA mara baada ya hafla ya kusaini hati ya makubaliano, Oktoba 28, 2025, Arusha.

About the author

Alex Sonna