Featured Kitaifa

DKT.NCHIMBI ATUA LITUHI NYASA-RUVUMA KUSAKA KURA ZA USHINDI WA KISHINDO ZA CCM

Written by Alex Sonna

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasili katika uwanja wa Kata ya Lituhi,jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma, leo Oktoba 19,2025 kwa ajili ya kuwahutubia Wananchi hao,ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya hadhara ya kampeni nchi nzima kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Lituhi, Balozi Dkt.Nchimbi amepewa baraka kutoka Nyumbani kwao kwa nafasi aliyopewa kuwa mgombea mwenza wa Urais kupitia CCM, zoezi hilo limeongozwa na Chifu wa himaya ya Nyasa na Katibu wa Machifu mkoa wa Ruvuma,Sadi Wabu.           

About the author

Alex Sonna