Featured Kitaifa

VIWANDA VITATU VILIVYOSIMAMA UZALISHAJI VYAFUFULIWA TANGA

Written by Alex Sonna

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah akikagua Mashine mpya katika Kiwanda kinachotarajiwa kuanza kazi Mwezi Januari cha Ply and Panel kinachomilikiwa na Bw. Hussen Moor, katika ziara yake ya kutembelea Viwanda hivyo vilivyopo mkoani Tanga, akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Mchatta, tarehe 13 Oktoba 2025

Na.Mwandishi Wetu-TANGA

Viwanda vitatu (3)vilivyosimama uzalishaji kwa sababu mbalimbali vimefufuliwa na vitaanza uzalishaji kamili Januari 2026 baada ya kukamilisha hatua mbalimbali ikiwemo ufungaji wa mitambo katika kipindi cha majaribio ya uzalishaji, Mwezi Disemba 2025.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah Oktoba 13, 2025 akiwa ameambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Rashid Mchatta pamoja na Wataamu wa Serikali wakati wa Ziara katika viwanda hivyo Jijini Tanga kwa lengo la kuangalia utekelezi wa jitihada mbali zinazoendelea katika kufufua Viwanda Mkoani humo ili kuifanya kuwa Tanga ya Viwanda.

Aidha, Dkt Abdallah ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Sera, Miongozo na kuwezesha ufufuaji wa Viwanda hivyo ambavyo vitaongeza ajira , Pato la Taifa pamoja na uchumi kwa ujumla

Viwanda vilivyotembelewa katika ziara hiyo ni Kiwanda cha Unique Steel Rolling kinachozalisha bidhaa za Chuma, Kiwanda cha Ply and Panel kinachotengeneza bidhaa za Mbao ikiwemo samani na magogo pamoja na Kiwanda cha African Harmony kinachozalisha bidhaa za Sabuni Amesema Dkt Abdallah.

Naye, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Rashid Mchatta ameahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara katika kuhakikisha Mkoa wa Tanga wenye raslimali nyingi yakiwemo madini pamoja na Bandari unakuwa na viwanda vingi vinavyofanya kazi ili kukuza uchumi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kiwanda Ply&Panel Limited na Unique Steel Rolling Bw. Hussein Moor pamoja na Meneja Raslimali Watu wa Bw African Harmony Bw. Ahmed Mtomola wameishukuru Serikali kwa kuwezesha ufufuaji wa viwanda hivyo na kuahidi Kuwa viwanda hivyo vitatoa ajira kwa watu wengi vitakapoanza kizalisha kikamifu

Nao Wafanyakazi katika Kiwanda cha African Harmony Bw. Edward Mnzava na Richard Mkama wamesema wamefurhishwa na hatua ya Serikali kuwezesha ufufuaji wa Viwanda hivyo vinavyotoa ajira za moj kwa moja na zisizo za moja kwa moj kwa Vijana wa Mkoa huo ambayo wengi walikuwa Mtaani kwa kukosa ajira.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu huyo katika Mkoa wa Tanga Oktoba 13, 2025 kwa lengo la kutembelea Viwanda vilivyofufuliwa katika jitihada za kufufua viwanda Mkoa wa Tanga.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amekutana na kufanya Mazungumzo na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Rashid Mchatta wakati wa ziara yake katika Mkoa huo Oktoba 13, 2025 kwa lengo la kutembelea Viwanda vilivyofufuliwa katika jitihada za kufufua viwanda Mkoa wa Tanga.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, akitembelea na kusikiliza maelezo kutoka kwa Mmiliki wa Kiwanda cha Unique Steel Rolling na Kiwanda cha Ply and Panel Bw. Hussen Moor, katika ziara yake ya kutembelea Viwanda hivy vilivyopo mkoani Tanga, akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Mchatta, tarehe 13 Oktoba 2025. Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kufufua viwanda katika mkoa huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah akikagua Mashine mpya katika Kiwanda kinachotarajiwa kuanza kazi Mwezi Januari cha Ply and Panel kinachomilikiwa na Bw. Hussen Moor, katika ziara yake ya kutembelea Viwanda hivyo vilivyopo mkoani Tanga, akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Mchatta, tarehe 13 Oktoba 2025

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, akitembelea na kusikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Rasilimali Watu wa Kiwanda cha African Harmony, Bw. Ahmed Mustapha, kinachozalisha sabuni ya unga aina ya Foma, alipotembelea kiwanda hicho kilichopo mkoani Tanga, akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Mchatta, tarehe 13 Oktoba 2025. Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kufufua na kuimarisha viwanda katika mkoa huo.

About the author

Alex Sonna