Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Ofisi ya Rais–Utumishi, Bi. Hilda Kabissa,akizungumza wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa maadili na utawala bora kati ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka za kitaaluma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo kilichoanza leo Oktoba 2,2025 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
OFISI ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesema imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu namna baadhi ya watumishi wa umma wanavyotoa huduma, ikiwamo matumizi ya lugha zisizofaa, kutojali utu na majibu yanayokatisha tamaa, kinyume na sheria, kanuni na maadili ya utumishi wa umma.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 2,2025 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Ofisi ya Rais–Utumishi, Bi. Hilda Kabissa, wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa maadili na utawala bora kati ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka za kitaaluma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo.
“Ofisi yangu imekuwa ikipokea mrejesho wa malalamiko kutoka kwa wananchi kutoridhishwa na namna ambavyo huduma zimekuwa zikitolewa, yakiwemo matumizi ya lugha zisizofaa kutoka kwa watumishi wa umma kinyume na sheria, kanuni, taratibu na mienendo ya maadili ya utendaji na maadili ya kitaaluma katika utumishi wa umma,” amesema Bi. Kabissa.
Amesema kuwa kikao hicho kinalenga kuwakumbusha watumishi wote kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya taaluma zao ili kutoa huduma bora, kwa kuzingatia weledi, uadilifu na uwajibikaji, hatua itakayosaidia kupunguza malalamiko na kuongeza imani ya wananchi kwa serikali.
Aidha, amewataka waajiri katika utumishi wa umma kuweka kipaumbele katika utoaji wa mafunzo ya maadili kwa watumishi wapya na waliopo, pamoja na kuepuka vitendo vya rushwa katika kazi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Bi.Kabissa pia amehimiza uwekezaji zaidi kwenye mifumo ya kielektroniki katika utoaji wa huduma ili kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi.
“Hali hii itasaidia kuongea uwajibikaji, uwazi na ufanisi kwa kupunguza mianya na vitendo vya rushwa kwa watumishi wa umma katika maeneo yenu pindi wanapotoa huduma kwa wananchi,”amesisitiza
Kadhalika, amewakumbusha watumishi na wananchi kusimamia utawala bora na kushiriki ipasavyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, kwa kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.
Naye, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili wa ofisi hiyo, Felster Shuli, amesema kuwa kikao hicho ni mwendelezo wa majadiliano ya kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa maadili ya utendaji na kitaaluma kilichoanza Septemba 2023.
“Katika siku hizi mbili za kikao kazi, tunatarajia kupokea mada tano zitakazojikita katika kuimarisha usimamizi wa maadili ya utendaji na kitaaluma katika utumishi wa umma,” amesema Bi. Shuli.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Ofisi ya Rais–Utumishi, Bi. Hilda Kabissa,akizungumza wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa maadili na utawala bora kati ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka za kitaaluma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo kilichoanza leo Oktoba 2,2025 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili wa ofisi hiyo, Felster Shuli,akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa maadili na utawala bora kati ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka za kitaaluma leo Oktoba 2,2025 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Ofisi ya Rais–Utumishi, Bi. Hilda Kabissa (hayupo pichani), wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa maadili na utawala bora kati ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka za kitaaluma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo kilichoanza leo Oktoba 2,2025 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Ofisi ya Rais–Utumishi, Bi. Hilda Kabissa,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa maadili na utawala bora kati ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka za kitaaluma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo leo Oktoba 2,2025 jijini Dodoma.