Featured Kitaifa

WATUMISHI IDARA YA KAZI NA AJIRA WAASWA KUONGEZA UFANISI

Written by Alex Sonna

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bi. Mary Maganga amewataka  watumishi wa idara ya Kazi na Kitengo cha Ajira  kuongeza ubunifu wakati wa kutimiza majukumu yao ,wito alioutoa Morogoro leo Oktoba 01,2025 wakati alipofungua kikao kazi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bi. Mary Maganga amewataka  watumishi wa idara ya Kazi na Kitengo cha Ajira  kuongeza ubunifu wakati wa kutimiza majukumu yao ,wito alioutoa Morogoro leo Oktoba 01,2025 wakati alipofungua kikao kazi.

 

Sehemu ya watumishi wa Idara ya Kazi na Kitengo cha huduma za ajira wakiwa kwenye kikao kazi leo Oktoba 01,2025 mjini Morogoro.

Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo (waliokaa mbele) toka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu wakiwa kwenye kikao kazi cha kujadili masuala ya Kazi na Ajira mjini Morogoro leo Oktoba 01,2025.

Kamishna wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bi.Suzan Mkangwa akieleza madhumuni ya kikao kazi cha kujadili masuala ya kazi na ajira kilichofanyika Morogoro leo Oktoba 01,2025 .
(Habari na Picha na OWM-KVAU)

Na OWM KVAU

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Mary Maganga amewataka Watumishi wa Ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ili kuongeza tija katika utoaji huduma kwa wananchi.

Bi. Mary amebainisha hayo leo Oktoba Mosi, 2025 mkoani Morogoro wakati alipofungua Kikao Kazi cha watumishi wa Idara ya Kazi na Kitengo cha Huduma za Ajira kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara hizo.

“Ninataka mfanye kazi kwa ushirikiano, ubunifu na uwajibikaji ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Serikali katika usimamizi wa masuala ya kazi na huduma za ajira nchini” alisisitiza Katibu Mkuu huyo.

Awali, Kamishna wa Kazi Ofisi hiyo, Bi. Suzan Mkangwa, amesema kuwa kikao hicho kimehusisha watumishi kutoka Mikoa yote nchini, ambapo watajadili masuala mbalimbali yanayohusu kazi.

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Ajira Bi. Josephine Matiro amesema kikao hicho ni fursa muhimu ya kujadili changamoto na mafanikio yaliyopo pamoja na kubadilishana uzoefu wa kitaaluma ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kikao hicho kimeandaliwa kwa lengo la kujadili kwa kina utekelezaji wa majukumu ya idara hizo pamoja na kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu namna bora ya kuboresha utendaji kazi .

About the author

Alex Sonna