Featured Kitaifa

MWENYEKITI INEC AKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2025 CHAMWINO

Written by mzalendo

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Septemba 25, 2025 ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma katika majimbo ya Chamwino na Mtera ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya majimbo hayo kutoka kwa msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

“Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura”

About the author

mzalendo