Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Iringa katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa tarehe 07 Septemba, 2025.
Na Mwandishi Wetu, Iringa
MAELFU ya wananchi wa Iringa leo Septemba 7, 2025 wameonesha hamasa na kumuunga mkono Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Samora.
Wananchi hao walijitokeza kwa wingi, wakipokea kwa shangwe hotuba ya Dkt. Samia iliyolenga kuendeleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuongeza ajira kwa vijana, kuimarisha vyama vya ushirika na kuboresha mazingira ya wajasiriamali wadogo.
Mapokezi hayo yameelezwa na wachambuzi wa siasa kama ishara ya dhahiri ya imani ya wananchi wa Iringa kwa Dkt. Samia na chama chake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Iringa katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa tarehe 07 Septemba, 2025.
Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa tarehe 07 Septemba, 2025.