Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ameukabidhi Uongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Magu Mkoa Mwanza, Ukumbi wa CCM baada ya kukamilisha maboresho na ukarabati mkubwa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika viwanja vya Ofisi ya CCM Magu, Dkt. Tax, alieleza kuwa amekamilisha ukarabati huo ikiwa ni utekelezaji wa maombi yaliyowasilishwa kwake na Kamati ya Siasa ya Wilaya ikiwa mchango wake kama Mwana CCM na Mwana Magu.
Aidha, amewakumbusha wana CCM Magu, kuendelea kutoa ushirikiano na kuwatia moyo kwa kuwaunga mkono Viongozi na wanachama wanaojitilea kuchangia katika shughuli za maendeleo katika jamii, ili kuwapa hamasa na kuondokana na mtazamo hasi kuwa wanaojitolea wanataka nafasi za Uongozi, Mitazamo ya aina hiyo hufifisha ari.
Naye Mwenyekiti wa CCM Magu, Komredi Enos Ndobeji Kalambo kwa niaba ya wana CCM Magu, alimshukuru Waziri Tax, kwa moyo wake wa kujitoa na kuainisha kuwa ni aina ya viongozi wachache wa mfano wa kuigwa.