Featured Kitaifa

CWT YAKOSHWA NA RAIS SAMIA KWA UTEKELEZAJI WA AHADI ZAKE KWA WALIMU NCHINI

Written by mzalendoeditor

KAIMU Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Dinna Mathamani,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 7,2022 jijini Dodoma wakimpongeza Rais Samia kwa kuendelea kutekeleza ahadi za walimu nchini.

Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Deus Seif,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 7,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Walimu pamoja na waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Kaimu Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Dinna Mathamani (hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari  leo Mei 7,2022 jijini Dodoma.

KAIMU Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Dinna Mathamani,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa  na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 7,2022 jijini Dodoma wakati wakimpongeza Rais Samia kwa kuendelea kutekeleza ahadi za walimu nchini.

………………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT),kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha maslahi ya walimu nchini ikiwemo upandishwaji wa madaraja na kutenga kiasi cha Shilingi Bilioni 55.57 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 809 za walimu.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 7,2022 jijini Dodoma na Kaimu Rais wa CWT Mwalimu Dinna Mathamani wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema tangu Rais Samia aiingie madarakani amefanya mambo mengi yaliyowagusa walimu na kuwapa ari ya kufanya kazi.

Mathamani amesema kuwa katika  upandishwaji madaraja katika mwaka wa fedha wa 2021/22 walimu wapatao 127000 wamepandishwa madaraja.

Amesema kuwa katika  suala la ajira ,katika kipindi cha mwaka mmoja tayari zaidi ya walimu 27,000 kwa awamu  pamoja na 12,000 wanaotarajiwa kuajiriwa itaongeza idadi ya walimu mashuleni na hivyo kuwapunguzia walimu vipindi na kuwawezesha kujiandaa vyema katika kufudisha wanafunzi vizuri.

Mathamani amesema kuwa katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia ujenzi wa miundombinu ya shule ambapo jumla ya madarasa 15,000 yamejengwa nchi nzima .

Amesema kupitia kujengwa kwa vyumba hivyo vya madarasa ,sasa wanafunzi hawasongamani madarasani na hivyo kuwafanya walimu kuongeza tija katika kufundisha wanafunzi.

“Suala hili limekuwa ni la msingi sana kwa Taifa,isipokuwa ombi letu kwa Serikali ni kuangalia tatizo la vyoo na nyumba za walimu kwani kuna baadhi ya maeneo hjata nyumba za kupanmga hakuna.”amesema Mathamani

Aidha amesema,CWT kinatambua jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutatua tatizo la walimu nchini ambapo jumla y ash.55.57 bilioni zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 809 na kuomba utekelezaji na usimamiiz thabiti wa jambo hilo ili liweze kutekelezeka kwa wakati na kupunguza changamoto hiyo.

Hata hivyo amesema kuwa wapo baadhi ya walimu waliokuwa na madai sugu lakini Serikali imelipa madai hayo na bado inaendelea kulipa madai hayo ya walimu .

“Tunaiomba Serikali ,kwa madai ambayo bado yapo yalipwe kwa wakati ili walimu watulie na shughuli ya kufundisha watoto badala ya kutumia muda mwingi kufiuatilia madai yao.”ameongeza

“Pia tumefarijika kwa ahadi ya Rais Samia ya kuongeza mishahara kwa watumishi ambao miongoni mwao ni walimu,kwa hiyo suala la mishara mipya tunalisubiri kwa hamu maana tunajua lipo katika hatua za utekelezaji.”

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Deus Seif, amesema kuwa  wao ndio waliopeleka mapendekezo Serikalini ya ajira kutokana na muitikio wa jamii katika kujitokeza kuandikisha watoto.

“Sisi Chama Cha Walimu tumejitahidi kuishawishi serikali watu wapate ajira kwa maana ukiangalia kuna walimu wanaofariki,kuna wanaostaafu halafu muitikio ukawa mkubwa wa jamii katika kuandikisha watoto na matokeo yake mwalimu mmoja anakuwa anazidiwa na vipindi”amesema Mwl Seif

About the author

mzalendoeditor