Featured Kitaifa

UWT YASISITIZA KUTAFUTA USHINDI WA KISHINDO KWA CCM UCHAGUZI MKUU 2025

Written by mzalendo

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) inaenda kufanya kazi ya kuzisaka Kura za Kishindo kwa Wagombea wake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Urais,Ubunge na Udiwani kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu Maalum wa UWT Taifa leo Tarehe 03, Agosti 2025 baada ya kutangazwa kwa Matokeo ya Kura za maoni ya Wagombea wa Ubunge na Uwakilishi Viti Maalum Makundi.

#KaziNaUtuTunasongaMbele
#MkutanoMkuuWaUWTtaifa2025

About the author

mzalendo