Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Julai 12,2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Julai 12,2025.
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Dk Best Magoma,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Julai 12,2025.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Julai 12,2025.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Julai 12,2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Mpango elekezi wa kuimarisha uwezo wa kufanya na kutumia tafiti za kiutendaji katika kuboresha huduma za afya ya msingi. Uzinduzi huo umefanyika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo iliyotolewa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kwa kutambua mchango wake katika uboreshaji wa huduma za afya nchini. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini Dodoma. (Anayekabidhi tuzo hiyo ni Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo kwaajili ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kwa kutambua uongozi wake mahiri na uwekezaji katika Sekta ya Afya. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri . (Anayekabidhi tuzo hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waganga Wakuu wa Mikoa mara baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
….
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango,amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuvitunza vifaa tiba kwenye vituo vyao kwa kuwa serikali imenunua kwa gharama kubwa ili vitumike kwa muda mrefu .
Dkt.Mpango ametoa maagizo hayo leo Julai 12,2025 wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini Dodoma.
Hata hivyo, amesema kuwa hali ya utunzaji wa kumbukumbu za matumizi ya dawa na vifaa tiba bado hairidhishi na kwamba hospitali na vituo vya afya havina utaratibu mzuri unaonesha matumizi sahihi ikiwamo bakaa ya vifaa hivyo hali inayotatiza usambazaji wa dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na kutoa mwanya wa wizi na matumizi yasiyosahihi.
“Ninawaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuimarisha eneo la kumbukumbu ili kuleta ufanisi katika utunzaji wa dawa na vifaa tib na kuepuka upotevu,”amesema Dkt.Mpango
Dkt.Mpango amesema kuwa kutopatikana kwa dawa muhimu kwenye hospitali na vituo vya afya ngazi ya tatu hasa za magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisukari na magonjwa ya moyo.
“Pendekezo langu kwa Wizara ya Afya kupitia upya mfumo wa utoaji wa dawa ili kuruhusu dawa hizi kupatikana katika ngazi hiyo pamoja na kuimarisha huduma za kliniki zinazotembea,”amesema Dkt.Mpango
kuhusu matumizi sahihi ya dawa hasa za maamivu na antibayotiki ambazo zikitumiwa kiholela madhara yake ni makubwa na zimebainika kusababisha usugu wa vimelea na kuathiri moyo, figo n aini.
“Nawataka ninyi kulipa kipaumbele zuala hili kwa kuongeza juhudi za utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya dawa ili kuisaidia jamii yetu kutambua na kuepuka madhara ya matumizi holela ya dawa,”alisema.
kuhusu kiapo cha kitaaluma cha uadilifu, Dkt.Mpango amesema kuwa utoaji wa huduma za afya zinazingatia kiapo cha maadili kinachohimiza kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili.
“Mkiwa wasimamizi wakuu wa utoaji huduma za afya kwenye maeneo yenu napenda kuwakumbusha mkasimamie kwa karibu wa kiapo cha maadili,”amesema
Aidha amesema katika kipindi cha miaka minne iliyopita serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha huduma ya afya ya msingi kwa kutoa Sh.trilioni 1.29 zimetumika.
Amewasihi waganga hao kuongeza chachu ya kufanikisha utekelezaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote kwa kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora kwenye vituo vyao vya kazi.
Amesema kuwa serikali imeweka kipaumbele cha rasilimali watu wenye weledi na imeajiri watumishi wapya 25,939 wa kada za afya katika ngazi ya msingi na kuongeza uwiano kati ya watoa huduma na wagonjwa na kusisitiza serikali itaendelea kutoa kipaumbele kwenye kada za kimkakati ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
“Tumieni mkutano huu kufanya tathmini ya utendaji wenu na kujiuliza ni kwa kiasi gani mmeweza kufikia kikamilifu malengo na matarajio ya wananchi na mtakapohitimisha mkutano huu mtoke na majibu na mikakati itakayotusaidia kutuongoza kufikia malengo ya utoaji huduma bora za afya kwa watanzania,”amesema
Kwa upande wake Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema kwa kutambua umuhimu wa kuboresha huduma za afya kulingana na miongozo iliyoweka na maelekezo ya kisera, serikali kupitia TAMISEMI, Afya kwa kushirikia na UNICEF imeandaa mpango elekezi wa uimarishaji uwezo wa kufanya na kutumia tafiti za kiutekelezaji katika kuboresha huduma za afya ngazi ya msingi kwa mwaka 2025 hadi 2030.
“Mpango huu lengo kuu ni kutoa mwelekeo kwa watumishi wa afya ngazi ya msingi kufanya tafiti na kutumia matokeo ya tafiti katika kutatua changamoto na kuboresha utoaji huduma bora za afya nchini,.”
Aidha Waziri Mchangerwa amesema kuwa kutoa huduma za afya ni kazi ya kizalengo inayohitajika kujitoa na kwamba hali waliyoikuta katika sekta hiyo ilikuwa na changamoto nyingi lakini kwa sasa imeboreka kwa kiasi kikubwa.
“Tulijipanga vizuri, changamoto tulizozikuta hazikuwa za kitanzania, matukio yaliyokuwa yakitokea katika maeneo yetu tulilazimika kufanya kazi kwa bidii , watendaji hawa wameimarika, tulifanya maamuzi magumu ili sekta hizi mbili ziweze kunyooka wapo walioondolewa kutokana na vitendo vya rushwa na ubadhirifu ambayo yalikuwa kinyume na misingi iliyowekwa, kwa sasa changamoto zilizokuwepo awali zimekuwa historia.”amesema Mchangerwa
Pia amesema kuwa umeandaliwa mpango wa mafunzo kwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya nchini ambao utawapa stadi za kiuongozi , kuwaimarisha kiuzalendo, na kifikra katika kuwahudumia watanzania katika kila kona ya nchi.
“Kwa miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Bajeti ya Wizara ya Afya imefikia trilioni 7.15 hivyo kufanya mageuzi makubwa ya utoaji huduma za afya nchini. Amesema Wizara inatarajia kuanzisha chaneli maalumu ya Afya (Afya Tv) ili iweze kutangaza taarifa zinazohusu afya kwa wananchi. “amesema Mhe. Mhagama
Pia ameongeza kwamba kwa sasa Tanzania inatarajia kuwa kuwa kituo cha umahiri wa matibabu ya upandikizaji ini, kituo cha umahiri matibabu ya mfumo wa mkojo, matibabu ya uzazi kwa wanaume, akili mnemba katika upasuaji, matibabu ya damu na upandikizaji uloto, matibabu ya figo, matumizi ya nyuklia katika matibabu ya saratani.
Awali Akisoma risala ya waganga wakuu wa mikoa na halmashauri, Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Dk Best Magoma,ameipongeza serikali kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika sekta ya afya kuanzia ngazi ya afya ya msingi.
Pia ameiomba Serikali kuhakikisha inapunguza uhaba wa nyumba za watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kukabiliana na dharura zinazowapata wananchi hususani nyakati za usiku.
“Kuwe na mpango wa motosha kwa watumishi wanaofanyakazi katika mazingira magumu hususani halmashauri za pembezoni hivyo kupunguza wimbi la kuhama kwa watumishi kwenda mijini na motisha iwe kwenye nyumba, usafiri na nishati.”amesema Dkt.Magoma
Mkutano huo wa siku tatu una kauli mbiu isemayo “Wajibu wa Waganga Wakuu wa Miko ana Halmashauri katika kuimarisha Ubora wa Huduma za Afya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote”