Featured Kitaifa

ZAIDI YA TRILIONI 1.7 ZATEKELEZA MAENDELEO MKOA WA SINGIDA – RC DENEGO

Written by mzalendoeditor

MKUU wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 4,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.

MKUU wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 4,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.

Na.Alex Sonna-DODOMA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  imewezesha Mkoa wa Singida kupokea kiasi cha shilingi trilioni 1.72 kwa kipindi cha miaka mitano (2020–2025). 
Fedha hizo zimetumika kugharamia shughuli za uendeshaji wa Serikali na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, miundombinu, maji, kilimo na utawala bora.
Akizungumza July 4, 2025, Jijini hapa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima  Dendego, ameeleza kuwa kati ya fedha hizo, Serikali Kuu imetoa jumla ya shilingi trilioni 1.055, sawa na wastani wa asilimia 95 ya bajeti iliyoidhinishwa kwa miaka yote mitano.
Amesema katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali ilitenga shilingi bilioni 180.25 na kufanikisha kutoa shilingi bilioni 153.80, sawa na asilimia 85 ya bajeti hiyo ambapo Mwaka uliofuata wa 2021/22 uliona ongezeko ambapo kati ya shilingi bilioni 199.42 zilizotengwa, Serikali ilitoa shilingi bilioni 202.44 – ikiwa ni utekelezaji wa asilimia 102. 
“Kwa mwaka 2022/23, kiasi cha shilingi bilioni 239.81 kilitengwa, na shilingi bilioni 221.66 zilitolewa, sawa na asilimia 92 ya bajeti. Mwaka 2023/24, Serikali ilitoa shilingi bilioni 241.65 kati ya bilioni 230.99 zilizopangwa, sawa na asilimia 105,” amesema na kuongeza;
Katika mwaka wa fedha wa mwisho wa kipindi hicho (2024/25), shilingi bilioni 236.29 zilitolewa kati ya bilioni 259.35 zilizotengwa, sawa na asilimia 91 ya bajeti, “amesema.
Amefafanua kuwa katika kipindi hicho hicho, Mkoa wa Singida umeongeza pato lake la ndani (Regional GDP) kutoka shilingi trilioni 2.709 mwaka 2020/21 hadi shilingi trilioni 3.398 mwaka 2024/25. Wastani wa pato la mwananchi mmoja mmoja umeongezeka kutoka shilingi 1,588,604 hadi shilingi 1,710,562.
“Mkusanyiko wa mapato kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) umeongezeka kwa kasi kutoka shilingi bilioni 11.9 mwaka 2021/22 hadi shilingi bilioni 30 mwaka 2024/25  sawa na ongezeko la asilimia 152,mapato ya ndani ya halmashauri za mkoa yameongezeka kutoka shilingi bilioni 14.6 hadi bilioni 24.8, ongezeko la asilimia 69.8,”amesema.

About the author

mzalendoeditor