Mbunge wa jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amechukua fomu ya maombi ya kugombea tena nafasi ya ubunge kwa kipindi kingine cha 2025/30 kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Fomu hiyo ameichukua leo Juni 30 2025 katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Ngara Mkoani Kagera.
Hata hivyo vyombo vya habari vilivyokuwepo katika eneo la tukio walipotaka mahojiano hakuwa tayari kuzungumzia chochote zaidi alisema wakati ukifika atazungumza.
