Featured Kitaifa

MAVUNDE ACHUKUA FOMU KUWANIA JIMBO LA MTUMBA

Written by mzalendoeditor

 

Na.Alex Sonna_DODOMA

WAZIRI wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Anthony Mavunde amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Mtumba.

Fomu hiyo amechukua leo Juni 28,2025 katika Ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma Mjini na kukabidhiwa fomu na Katibu wa CCM Wilaya ya hiyo,Sophia Kibaba.

Mara baada ya kuchukua fomu hiyo,Mavunde amesema ametekeleza haki yake ya kikatiba ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Mtumba.

“Nimefika hapa kufuata haki yangu ya kikatiba ya kugombea kwenye Jimbo la Mtumba, hapo awali lilikuwa Jimbo la Dodoma Mjini.Leo nipo hapa kuomba ridhaa imani yangu yale yote ambayo Chama imeelekeza nitazingatia kwani nimelelewa na CCM naelewa misingi yote.Kama nitapata ridhaa nitaenda Jimbo la Mtumba,”amesema Mavunde.

 

About the author

mzalendoeditor