WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera,Bunge na Uratibu William Lukuvi,akizungumza wakati akizindua Bodi Mpya ya Mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (AIDS Trust Fund-ATE) hafla iliyofanyika leo Juni 26,2025 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera,Bunge na Uratibu William Lukuvi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (AIDS Trust Fund-ATE) hafla iliyofanyika leo Juni 26,2025 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera,Bunge na Uratibu William Lukuvi,amesema Serikali imeendelea kuongeza nguvu kubwa katika juhudi mbalimbali za kutokomeza maambukizi ya VVU na UKIMWI nchini.
Mhe.Lukuvi ameyasema hayo leo Juni 26,2025 jijini Dodoma wakati akizindua Bodi Mpya ya Mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (AIDS Trust Fund-ATE).
Amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha huduma za kinga,tiba na matunzo pamoja na kuendeleza ushirikiano wa ndani na nje ya nchi katika kuboresha mifumo ya afya.
“Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha dhamira ya kweli katika kuondoa kabisa maambukizi mapya ya VVU kwa kuwekeza kwenye huduma bora za afya na kuhimiza ushirikiano wa wadau”amesema Mhe.Lukuvi
Aidha Waziri Lukuvi ameitaka Bodi hiyo Mpya kuhakikisha inabuni vyanzo vya kimkakati vya fedha za utekelezaji wa afua za mapambano ugonjwa wa UKIMWI kutokana na upungufu wa asilimia 40 wa fedha za wahisani.
Kwa upande wake Mwnyekiti wa Bodi ya ATE ,Sabasaba Moshingi,amesema kuwa bodi hiyo itafanya kazi kwa weledi na ubunifu ili kuongeza vyanzo vya mapato.