Featured Kitaifa

KAMATI YA USHAURI MRADI WA EMA YAKUTANA DODOMA

Written by mzalendoeditor

Bw. Wanjara Jandwa kutoka Kitengo cha Huduma za Sheria cha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akiongoza Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kitaasisi wa Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) jijini Dodoma leo Juni 25, 2027.

Wajumbe wakiwa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kitaasisi wa Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) jijini Dodoma leo Juni 25, 2027.

….

Kamati ya Ushauri ya Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kitaasisi wa Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) imekutana kwa ajili ya kujadili na kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 jijini Dodoma leo Juni 25, 2027.

Kikao hicho kimeongozwa na Bw. Wanjara Jandwa kutoka Kitengo cha Huduma za Sheria cha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambaye aliwapongeza kwa kazi nzuri ya kutoa maoni yenye kujenga.

Bajeti hiyo iliyowasilishwa na Mratibu wa Mradi Bw. Richard Masesa imejadiliwa na wajumbe walioshiriki kikao hicho kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, NEMC, Wizara za kisekta na halmashauri.

Mradi wa EMA unaosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, unafadhiliwa na Serikali ya Sweden kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA), unakusudia kushughulikia changamoto kuu za mazingira na kuondoa vizuizi vya kisekta vilivyopo katika Wizara na mamlaka maalumu za kisheria na kuongeza wigo wa utendaji.

Kwa mantiki hiyo, mradi huo ni nyenzo mojawapo ya kuboresha uratibu wa usimamizi wa mazingira nchini unaokusudia kushughulikia changamoto kuu za mazingira.

About the author

mzalendoeditor