Featured Kitaifa

SERIKALI YAJENGA BANDARI NYINGINE ZANZIBAR KULINDA MAZINGIRA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Juni 25, 2025.

…….

SERIKALI inajenga bandari nyingine nje ya Manispaa ya Mtwara Mikindani itakayotumika kusafirisha bidhaa chafuzi kwa mazingira na afya kama vile saruji na makaa ya mawe, ili magari yote yanayobeba makaa ya mawe kupita nje ya manispaa kuelekea bandarini. 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Juni 25, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Tunza Malapo, aliyetaka kujua Serikali imejipangaje kudhibiti vumbi la makaa ya mawe yanayosafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Khamis alisema Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Ofisi ya Makamu wa Rais zinashirikiana kutekeleza mradi huo katika eneo la Kisiwa Mgao.

Alisema kuwa katika kutekeleza mradi huo itatumika mitambo miwili yenye uwezo wa kupakia tani 600 kwa saa ambayo ina mikanda maalum (conveyor belt) kwa ajili ya kupakia mzigo kwenye meli.

Mhe. Khamis alitaja hatua nyingine ni kuweka nyavu za kuzuia vumbi, kuhakikisha magari yote yanayosafirisha makaa ya mawe yanafunikwa ili kuzuia vumbi lisisambae kwenye mazingira na kunyunyuzia maji mara kwa mara katika eneo la hifadhi.  

Akijibu swali la nyongeza la mbunge huyo kuhusu Serikali imetoa elimu na vifaa kwa wafanyakazi na vibarua kujikinga na vumbi kutokana na makaa ya mawe, Naibu Waziri alisema Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), TAMISEMI, Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) na Bandari zinashirikiana kutoa elimu ya kutumia vifaa vya kujikinga wasipate madhara.

“Pamoja na kutoa elimu tunawaelekeza na kuwasimamia wamiliki wote wa magari yanayoyeba makaa ya mawe kuyafunika ili vumbi lisitoke na kuchafua mazingira na afya kwa binadamu,” alisema Naibu Waziri Khamis.

Kwa upande mwingine, Mhe. Khamis alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imechukua hatua ya kujenga na kukarabati baadhi ya bandari zikiwemoya Mpigaduri na Mangapwani hatua itayosaidia kupunguza msongamano na kutenganisha sehemu ya kupakia na kupakua mizigo na abiria.

Alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Amani Mhe. Abdul Yussuf Maalim aliyeuliza hatua za kidhibiti vumbi kutokana na bidhaa za saruji zinazoingia katika Bandari ya Zanzibar.

About the author

mzalendoeditor