Featured Kitaifa

DKT. CHAULA ATETA  NA MKURUGENZI MRADI WA USAID AFYA YANGU 

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawakilishi wa Mradi wa USAID Afya Yangu akiwemo Mkurugenzi Mradi Dkt. Marina Njelekela (kulia) na Meneja Mradi Nyantito Machota (kulia nyuma) walipofika ofisini kwake jijini Dodoma kujitambulisha wengine ni Wakurugenzi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum.
……………………………………
Na WMJJWM -Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amekutana na wadau kutoka Mradi wa USAID Afya Yangu kenye Ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Ujumbe kutoka Mradi wa USAID Afya Yangu uliongozwa na 
Mkurugenzi wa Mradi Dkt. Marina Njelekela na Meneja Mradi Nyantito Machota.
Katika kikao hicho Dkt. Zainab Chaula na Wawakilishi wa Mradi wa USAID Afya Yangu wamejadiliana mambo kadhaa ikiwepo uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi na masuala ya Kijinsia.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kukutana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha inaweka mikakati na Mipango ya kuwahudumia wananchi.

About the author

mzalendoeditor