Featured Kitaifa

MEJA JENERALI MABELE AWAONDOA HOFU VIJANA JKT, MAFUNZO SIO MATESO

Written by mzalendo
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati akifungua mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni nishati safi mwaka 2025 katika kambi ya JKT Makutupora leo Juni 18,2025.
Mkuu wa tawi la mafunzo JKT Kanali Longinus Nyingo akizungumza wakati akifungua mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni nishati safi mwaka 2025 katika kambi ya JKT Makutupora leo Juni 18,2025.
Mkuu wa Kikosi JKT Makutupora Kanali Festo Mbanga, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni nishati safi mwaka 2025 katika kambi ya JKT Makutupora leo Juni 18,2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele akiwasili kwenye ufunguzi wa mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni nishati safi mwaka 2025 katika kambi ya JKT Makutupora leo Juni 18,2025.
Vijana waliojiunga na mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni nishati safi mwaka 2025 katika kambi ya JKT Makutupora.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza na kuimba na vijana waliojiunga na mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni nishati safi mwaka 2025 katika kambi ya JKT Makutupora leo Juni 18,2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele akiwa na makamada wengine wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni nishati safi mwaka 2025 katika kambi ya JKT Makutupora leo Juni 18,2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele akiwaaga vijana waliojiunga na mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni nishati safi mwaka 2025 katika kambi ya JKT Makutupora leo Juni 18,2025.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amewatoa hofu vijana wanaojiunga na mafunzo ya  jeshi kuwa hakuna mateso kwani mafunzo hayo yanalenga kuwajenga kuwa wakakamavu na wazalendo kwa taifa.
Mkuu huyo wa JKT ameyasema hayo leo Juni 18,2025 Jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni nishati safi mwaka 2025 katika kambi ya JKT Makutupora kuashiria ufunguzi wa Mafunzo hayo nchini. 
“Hatufundishi uzalendo huko mlikotoka nyinyi ni wazalendo,  tunakuza moyo wa kizalendo, tunataka tuwajengee nidhamu, japo tunaamini kule mlikotoka mlikuwa na nidhamu njema, tunataka tuendeleze tuwajengee muishi maisha ya nidhamu, tuwape ukakamavu kwaajili ya kuilinda nchi yetu, muwe majasili muweze kujiamini, tuwajengee moyo wa kupendana.
Aidha amewataka vijana hao pamoja na wakufunzi wao kujiepusha na mambo yasiyotakiwa hasa katika kipindi hiki cha mafunzo ikiwemo mapenzi, ulevi na vitendo vya wizi.
Mkuu huyo pia amewaomba vijana hao kuwa tayari na huru kueleza mambo yote yatakayokuwa kinyume na taratibu za mafunzo hayo kwani wamewatengenezea utaratibu mzuri wa kutoa taarifa.
“Chochote kile ambacho unaona kinakwenda nje ya taratibu za mafunzo, unaona kabisa haya sio mafunzo mtu anakuchukua peke yako anakupeleka polini, unaenda kufanya nini unajua kabisa hiyo ni nje ya taratibu za mafunzo kwahiyo muwe tayari kutoa taarifa kwa mtu yeyote anayeleta kitu ambacho ni kinyume cha taratibu za mafunzo,”amewaomba.
Amesema hilo litawasaidia kuchukua hatua za haraka pale kitu cha namna hiyo kinapokuwa kimetokea, na kurudia kuwa wasitishwe na mtu wa aina yeyote kwa maana Jeshi la Kujenga Taifa yeye ndiye yuko juu na yeye ndiye kuwaambia hivyo.
Kwa upande wake Mkuu wa tawi la mafunzo JKT Kanali Longinus Nyingo amesema muitikio wa vijana hao ni ishara tosha kuwa wao ni wasikivu, wanyenyekevu na wazalendo na namna walivyoonesha morali siku ya leo inaonesha namna ambavyo wako tayari kupokea mafunzo hayo.
“Mafunzo haya kwa mujibu wa sheria yanalenga mambo mbalimbali ikiwemo kuwapa mafunzo ya awali ya kijeshi ili kuwapa uwezo wa kuwa walinzi wa taifa,”amesema. 
Naye Mkuu wa Kikosi JKT Makutupora Kanali Festo Mbanga amesema kuwa yapo mahitajio mengi ambayo kwa maelekezo ya Mkuu wa JKT aliyoyatoa tayari wameyapata ni pamoja na vitanda, magodoro, mahanga, madawa na wakufunzi wameandaliwa vizuri kwaajili kuendesha kozi kwa kufuata vigezo na maelekezo yote ambayo yametolewa.
“Mimi mkuu wa kikosi kwa niaba ya maafisa, askari na vijana wote tulioko hapa ambao tutasimamia hii kozi, tukuahidi kwamba vigezo ambavyo vimewekwa kwaajili ya kozi hii vinazingatiwa na taratibu zote zitazingatiwa ili tuendelee kutunza taswira nzuri ya mafunzo haya kwa vijana wa kitanzania, “amesema. 

About the author

mzalendo