Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa,akiwasilisha leo Mei 15,2025 bungeni jijini Dodoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
….
WIZARA ya Uchukuzi imetaja mafanikio iliyoyopata katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita ikiwemo kuanza uendeshaji wa reli ya SGR na Kuendelea kwa Ujenzi katika Vipande mbalimbali vya SGR.
Mafanikio hayo yametajwa bungeni Dodoma na Waziri wa Wizara hiyo,Prof Makame Mbarawa wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Prof Mbarawa amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefungua soko la nje kwa kuhakikisha reli ya SGR inaunganisha nchi jirani ikiwemo Jamhuri ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Amesema katika kutekeleza hilo Serikali imefanikisha kupata fedha za ujenzi wa reli ya SGR kutoka Tabora – Kigoma (Km 506) ambayo itafungua mipaka ya biashara na nchi ya Demokrasia ya Congo kupitia Ziwa Tanganyika (Kigoma) na ujenzi wa reli ya SGR kutoka Uvinza – Musongati (km 240) ambapo mkataba wa ujenzi wa reli hio umesainiwa Januari 29 2025.
Ameyataja mafanikio mengine ni ununuzi wa ndege ambapo Serikali imeendeleza utekelezaji wa Mpango wa Ufufuaji wa Shirika la Ndege ATCL kwa kununua ndege saba (7) na kufanya kuwa na ndege 15.
Waziri Mbarawa ameyataja mafanikio mengine ni Kuendelea Kuboresha Huduma za Usafiri na Usafirishaji katika Maziwa Makuu, UboUdhibiti wa Usafiri wa uboreshaji wa Huduma za Bandari.