Featured Kitaifa

VIPIMO 1,013,859 VIMEKAGULIWA 10,898 VILIREKEBISHWA 761 VILIKATALIWA

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiwasilisha leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Na.Alex Sonna-DODOMA
KUPITIA  Wakala wa Vipimo(WMA), Wizara ya Viwanda na Biashara   imekagua na kuhakiki vipimo 1,013,859 sawa na asilimia 99.2 ya lengo la vipimo 1,022,342 vilivyopangwa kukaguliwa kwa mwaka.
Hayo yameelezwa leo  Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma  na Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara,Dkt.Selemani Jafo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Jafo amesema kati ya vipimo hivyo, vipimo 10,898 vilirekebishwa na vipimo 761 vilikataliwa.
Amesema WMA imeendelea kufanya kazi ya udhibiti wa bidhaa zilizofungashwa mipakani na bandarini katika vituo vya ukaguzi 13 ambavyo ni Sirari, Mtukula, Namanga, Holili, Tunduma, Tarakea, Horohoro, Kasumulu, Kwara na Bagamoyo, Manyovu, na Mbweni na Temeke.

About the author

mzalendoeditor