Featured Kitaifa

MAHAREGE,NJEGERE,MATUNDA VYAPATA SOKO KIMATAIFA

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiwasilisha leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Na.Alex Sonna-DODOMA
Wizara ya Viwanda na Biashara  imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinapata masoko ya kikanda na kimataifa.
Hayo yameelezwa leo Mei 14,2025 bungeni  Dodoma na Waziri wa Wizara hiyo,Dkt.Selemani Jafo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Jafo amesema katika kutekeleza Mfumo Rahisi wa Ufanyaji Biashara kwa Wafanyabiashara Wadogo (STR) wanaovuka mipaka ya Tanzania na Zambia, jumla ya bidhaa 51 zilikubalika kuingia katika mfumo rahisi wa ufanyaji biashara kwa wafanyabiashara wadogo wanaovuka mpaka wa Tanzania na Zambia kutoka bidhaa 22 za awali.
Amesema bidhaa hizo mpya ni pamoja na maharage, njegere, matunda mbalimbali, viazi mviringo, soya na mboga mboga za kukausha.  Aidha, kwa upande wa Tanzania na Malawi, majadilino ya uwili ya kuanzisha Mkataba wa Taratibu Zilizorahisishwa za Kiforodha.
“ Jumla ya bidhaa 61 za viwandani na kilimo zilikubalika kuingia katika mfumo huo wa STR; Ukomo wa thamani ya bidhaa wa dola za Marekani 2000 umekubalika; na Idadi ya uvukaji usio na ukomo usiozidi ukomo wa thamani  hiyo umekubalika pia,”amesema Waziri Jafo

About the author

mzalendoeditor