Featured Kitaifa

WAZIRI AWESO AOMBA BUNGE KUIDHINISHA BAJETI YA TRILIONI 1.01

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akiwasilisha leo Mei 8,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026 .
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akiwasilisha leo Mei 8,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026 .
……

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya Shilingi 1,016,894,958,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2025/26. Kati ya fedha hizo, Shilingi 73,779,579,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 943,115,379,000 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Amefafanua mbele ya Bunge, Waziri Aweso alieleza kuwa kati ya fedha za matumizi ya kawaida, Shilingi 18,081,382,000 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia matumizi mengineyo (OC), huku Shilingi 55,698,197,000 zikiwa zimepangwa kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wa Wizara ya Maji, Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mfuko wa Taifa wa Maji, pamoja na Chuo cha Maji.

Kwa upande wa bajeti ya maendeleo, Waziri Aweso alibainisha kuwa Shilingi 340,463,656,000 sawa na asilimia 36.1 ya fedha hizo ni fedha za ndani, huku Shilingi 602,651,723,000 sawa na asilimia 63.9 zikiwa ni fedha za nje kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo.

Waziri Aweso amesisitiza kuwa bajeti hiyo inalenga kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, hasa katika kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji mijini na vijijini.

About the author

mzalendoeditor