Msemaji wa sekta ya Utumishi na Utawala bora na Muungano kutoka chama ACT -Wazalendo Pavu Abdalah akizungumza na waandishi wa habari Jijin Dar es Salaam.
*****************
Na Magrethy Katengu,Dar es Salaam
Chama Cha ACT wazalendo kimeiomba serikali kuendelea kuwalipa Watumishi wa Umma malimbikizo ya mishahara na stahiki stahiki zao ambapo mpaka sasa imefikia kiasi cha bilioni 429.08.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam Msemaji wa sekta ya Utumishi na Utawala bora na Muungano kutoka chama ACT -Wazalendo Pavu Abdalah mara baada ya kusikiliza ripoti Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora ilisomwa bungeni Aprili 21 mwaka huu ambapo amesema mishahara ya Watumishi wa Umma haijapandishwa toka mwaka 2014.
“Ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi ni takwa la kisheria wala si la kiongozi mmoja katika Nchi kauli za huko nyuma zinaonyesha serikali iliahidi kuongeza mishahara baada ya kukamilisha uhakiki wa wafanyakazi ambao ungefanyika ndani ya miezi miwili kisha ikaendele kulipa madai ya malimbikizo ya madeni lakini haikufanya hivyo”. Amesema Pavu.
Hata hivyo wameiomba Serikali kupambana na mikakati sera zake kwa kujali kulipa stahiki za malimbikizo ya madai yao itawasaidia kumudu gharama za maisha kwa hali ya sasa ambapo bei za vitu vimepanda ikilingalishwa na hapo awali.
Aidha cha chama Cha ACT wazalendo kimeomba serikali kuhakikisha wanaongeza jitihada za makusudi kupambana na wezi wa njia ya mitandao ambao kila siku wananchi wamekua wakitapeliwa.
“Suala hili limekua kilio cha watu kila kukicha kwa kupigiwa simu na wakati mwingine kutapeliwa kupitia ujumbe wa maneno kwa njia ya simu”. Amesema.