Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya afya kitaifa pamoja na kuzindua mfuko maalum wa ufadhili wa masomo kwa Madaktari Bingwa na Bobezi Leo Aprili 8,2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya afya kitaifa pamoja na kuzindua mfuko maalum wa ufadhili wa masomo kwa Madaktari Bingwa na Bobezi Leo Aprili 8,2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya,Dk Godwin Molel,akizungumza wakati wa Kilele Cha Wiki ya Afya kitaifa Leo Aprili 8,2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Dk Seif Shekilaghe,akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya kitaifa pamoja na kuzindua mfuko maalum wa ufadhili wa masomo kwa Madaktari Bingwa na Bobezi Leo Aprili 8,2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama,(hayupo Pichani) wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya afya kitaifa pamoja na kuzindua mfuko maalum wa ufadhili wa masomo kwa Madaktari Bingwa na Bobezi Leo Aprili 8,2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
NA.Alex Sonna_DODOMA
SERIKALI imendelea kuboresha huduma za afya kwa kuongeza idadi ya hospitali zenye majengo ya kutolea huduma za dharura (EMD) kutoka 7 hadi kufikia 116 ndani ya miaka minne ikiwa ni ongezeko la Hospitali 109.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo leo Aprili 8, 2025 wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya afya kitaifa pamoja na kuzindua mfuko maalum wa ufadhili wa masomo kwa Madaktari Bingwa na Bobezi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Waziri Mhagama amesema kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya kutolea huduma za dharura kunapunguza vifo na kuokoa maisha kwa wagonjwa wa dharura na wa ajali.
Kuhusu huduma ya magari ya wagonjwa Waziri Mhagama amesema idadi ya magari ya imeongezeka kutoka 540 mwaka 2020 hadi 1,267 jambo linalorahisisha huduma za dharurana kuwafikia wananchi wenye changamoto za afya.
“Magari haya yanakwenda kusaidia kusafirisha watu wenye changamoto za afya wakiwemo akinamama wenye changamoto za uzazi kwa haraka na kuwafikisha katika huduma za rufaa na hivyo kupunguza adha kwa wananchi na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika,” amesema Mhe. Mhagama.
Aidha, Waziri Mhagama amezishukuru Sekta binafsi nchini kwa kuunga mkono Serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi kuanzia ngazi ya msingi hadi ya Kitaifa.