Featured Kitaifa

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA WAFANYABIASHARA- KIGAHE 

Written by mzalendoeditor
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe,akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa, Wilaya, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Wafanyabiashara na Wamachinga mkoani Iringa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Iringa,wakati akihitimisjha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri  wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe,(hayupo pichani) wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa, Wilaya, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Wafanyabiashara na Wamachinga mkoani Iringa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Iringa,wakati akihitimisjha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.

Na.Mwandishi Wetu-IRINGA
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe, amehitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Iringa, ambapo ameagiza kurudishwa kwa Wamachinga (wafanyabiashara wadogo) katika maeneo rasmi yaliyotengwa na Serikali kwa ajili ya biashara zao.
‎Naibu Waziri huyo, ameeleza kwamba maeneo rasmi ya Wamachinga kufanyia biashara zao ni soko la Mlandege, Lavera na Magari mabovu.
‎Naibu Waziri Kigahe ameyaagiza hayo  katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Iringa na kuwakutanisha Viongozi mbalimbali wa Mkoa, Wilaya, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Wafanyabiashara na Wamachinga mkoani Iringa.
‎Mhe.Kigahe ameeleza kuwa ni muhimu kwa wafanyabiashara wadogo kufanya shughuli zao katika maeneo rasmi ili kuepuka usumbufu na kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria na taratibu za biashara nchini.
 “Nawataka Wamachinga ambao wamekuwa wakifanya biashara katikati ya mji wa Iringa kurudi katika maeneo yaliyotengwa kama vile soko la Mlandege, Lavera, na maeneo mengine ya biashara rasmi.”amesema Mhe.Kigahe
Aidha ‎Mhe.Kigahe amewaonya wafanyabiashara hao kuwa Serikali itachukua hatua kali kwa wale watakaoshindwa kufuata maagizo hayo na kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Hata hivyo ‎ameongeza kuwa Serikali itaendelea kufanya juhudi za kuboresha miundombinu katika maeneo rasmi ya biashara ili kufanya mazingira ya biashara kuwa bora na salama kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.
‎“Serikali imejizatiti kutenga maeneo rasmi kwa wafanyabiashara wadogo. Ni muhimu wafanyabiashara hawa waendelee kufanya kazi zao kwa ufanisi katika maeneo hayo rasmi. Ni lazima wahamie huko na kuzingatia sheria za biashara. Maeneo yasiyoruhusiwa ni hatari kwa biashara na usalama wao,” amesema Kigahe.
‎Katika ziara yake, Kigahe pia ametembelea viwanda mbalimbali mkoani Iringa ili kuona hali ya uzalishaji na maendeleo ya viwanda na kuangalia maendeleo ya viwanda vinavyozalisha bidhaa tofauti na kutoa ajira kwa wananchi wa mkoa wa Iringa.
‎Awali Naibu Waziri Kigahe alitembelea kiwanda cha chai kilichopo Mufindi, mkoani Iringa ambapo alizungumzia changamoto zinazowakumba wakulima na wafanyakazi wa kiwanda hicho kwa kutokulipwa stahiki zao ndani ya miezi mitatu.
‎Kufuatia madai hayo, Naibu Waziri Kigahe ameiagiza kampuni ya DL, inayomiliki kiwanda hicho kuhakikisha kuwa wakulima na wafanyakazi wa kiwanda hicho wanalipwa madai yao bila kusuasua.
‎“Ni muhimu kwa kiwanda hiki kuhakikisha kuwa wakulima na wafanyakazi wake wanapata stahiki zao kwa wakati. Serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kuwa haki za wafanyakazi na wakulima zinazingatiwa,” amesema Kigahe.
‎Pia, Kigahe ametembelea kiwanda cha maji cha Mkwawa, kiwanda cha mbao cha Evergreen kilichopo Mufindi, na kiwanda cha Lonze kilichopo Lungemba, Mafinga ili kuangalia hali ya uzalishaji na changamoto zinazowakabili viwanda hivyo.
‎Lakini pia Mhe. Kigahe amewataka viongozi wa viwanda hivyo kuhakikisha kuwa wanazingatia mazingira bora ya kazi, kuboresha miundombinu na kuongeza tija ya uzalishaji ili viwanda viweze kuchangia zaidi katika uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla.
‎“Mafanikio ya viwanda ni mafanikio ya Taifa. Ni lazima tuhakikishe kuwa viwanda vyetu vinatoa bidhaa bora, vinatoa ajira kwa vijana na vinaongeza mapato kwa wananchi. Ni muhimu kuwa na usimamizi bora katika viwanda vyetu,” amesema Kigahe.
‎Katika ziara hiyo, Kigahe amezungumzia pia umuhimu wa Serikali kuendelea kutoa fursa kwa viwanda vidogo na vya kati ili kuhakikisha kuwa wanapata huduma za umeme, maji, na miundombinu ya usafirishaji ili kufanikisha uzalishaji wa bidhaa.
‎Katika hatua nyingine Mhe. Kigahe amewahimiza wamiliki wa viwanda kuwekeza katika teknolojia mpya ili kuongeza tija na ubora wa bidhaa zinazozalishwa.
‎Kigahe ameongezea kuwa serikali imejizatiti kuanzisha na kukuza viwanda vya BBT ili kuimarisha uchumi wa Taifa na kuleta maendeleo kwa wananchi na kusema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi na wananchi katika kuhakikisha kuwa viwanda vinapata huduma bora na mazingira salama ya kufanya kazi.
‎Ziara ya Naibu Waziri Kigahe mkoani Iringa imejikita zaidi katika kuhamasisha uboreshaji wa mazingira ya biashara, kuhimiza uwajibikaji wa wamiliki wa viwanda, na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wadogo wanapatiwa huduma bora.
‎Na katika kuhakikisha hayo yote yanafanikiwa Waziri Kigahe ameahidi kuendelea kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake ili kuhakikisha kuwa viwanda vya Iringa vinakuwa na tija na wafanyabiashara wadogo wanakuwa na fursa za kukuza biashara zao katika mazingira bora.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Kheri James aliyekuwepo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, amemshukuru sana Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
‎Mhe. Exaud Kigahe kwa kufanya mkotano na wafanyabiashara kwa lengo la kuwasiliza maoni, changamoto na ushauri wa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara.

About the author

mzalendoeditor