Featured Kitaifa

MAJALIWA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 53 YA KIFO CHA KARUME

Written by mzalendoeditor

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Aprili 7, 2025 ameshiriki Maadhimisho ya  Kumbukumbu ya Miaka 53 ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume kwenye Afisi Kuu ya CCM Kisiwandua  Zanzibar.

Viongozi wengine aliohudhuria ni pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Stephen Wasira, Mjane wa Hayati Karume, Mama Futuma Karume, Watoto ya Hayati Karume, Amani Abedi Karume na Balozi, Ali Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein.

About the author

mzalendoeditor